Watu wawili wamepoza maisha katika ajali ya Ndege iliyotokea mapema leo huko Seronera, Serengeti mkoani Mara. Ndege hiyo mali ya Kampuni ya Auric Air inayodaiwa ilikuwa ikiruka kutokea uwanja mdogo wa Seronera kuelekea eneo la Grumet ilianguka wakati ikitaka kuruka.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Mawasiliano wa TANAPA, Pascal Shelutete amesema, ndege hiyo yenye namba ya kuruka 5H-AAM ilikuwa inaendeshwa na Nelson Mabeyo,Shelutete amebainisha kuwa ndege hiyo ilipoteza uelekeo na kuanguka ilipokuwa ikitaka kuruka kuelekea Grumet ikiwa na abiria mmoja.
Taarifa kamili zitafuata.
Taarifa kamili zitafuata.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2kza4o7
via

