Rais Samia na Dkt.Nchimbi wa CCM Wateuliwa Kugombea Urais
TUMEÂ Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewateua Rais Samia Suluhu Hassan na mgombea mwenza wake, Dk Emmanuel Nchimbi, kugombea nafasi ya urais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.
Akizungumza leo Agosti 27, 2025 jijini Dodoma, Mwenyekiti wa INEC, Jaji Mstaafu Jacobs Mwambegele, amesema wagombea waliopendekezwa na CCM wametimiza masharti yote ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo kuthibitishwa rasmi kuwania nafasi hizo.
“Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inawateua Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dk Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema Jaji mstaafu Mwambegele.
Uteuzi huo unawafanya Samia na Nchimbi kuingia rasmi katika kinyang’anyiro cha urais kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu ambao kampeni zake zinatarajiwa kuanza kesho Agosti 28, 2025.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






