RAIS MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MABALOZI WATATU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

7 years ago122 Views

Rais John Magufuli Januari 16, 2019,  amepokea hati za utambulisho wa mabalozi watatu wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.


Mabalozi hao ni Cho Tae-ick wa Korea Kusini, Glad Munthali wa Malawi na Antonio Cesar wa Brazil, wote wakichukua nafasi za watangulizi wao ambao walimaliza muda wao Desemba, mwaka jana.

Cho Tae-ick ambaye aliwasili nchini Desemba 14, 2018, amechukua nafasi ya mtangulizi wake, Balozi Song Geum Yong ambaye alimaliza muda wake.

Naye Glad Munthali ambaye aliwasili nchini Desemba 28, amechukua nafasi ya mtangulizi wake, Balozi Hawa Ndilowe ambaye muda wake ulikwisha Julai, 2018 na kuondoka nchini mwishoni mwa mwaka jana.

Kwa upande wake, Cesar aliwasili nchini Januari 3 na kuchukua nafasi ya Balozi Carlos Alfonso Puente ambaye pia muda wake ulikwisha Desemba 2018. Mabalozi wote watawakilisha nchi zao kwa muda wa miaka mitatu.

Katika mazungumzo yao na Rais Magufuli, walijadili kuhusu kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na nchi zao na Rais Magufuli aliwaeleza dira ya Serikali yake na kuwakaribisha kushiriki katika biashara na uwekezaji hapa nchini.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Serikali akiwemo Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Damas Ndumbaro.

from CCM Blog http://bit.ly/2HhvG2U
via

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Previous Post

Next Post

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.