RAIS KIKWETE AFUNGUKA: “NISINGEKUWA RAIS NINGEKUWA MSANII MKALI SANAWA BONGO FLEVA.”………MSIKIE HAPA

Admin Updates10 years ago5 Views

Mpekuzi blog

RAIS
Dkt. Jakaya Kikwete, ametamba kuwa angakuwa msanii wa muziki wa kizazi
kipya basi angelikuwa wa “BongoFleva” kutokana na kuwa na sauti nzuri
yenye kumudu kuimba nyimbo kwa ufasaha zaidi.



Kauli
hiyo aliitoa  jana jijini Mwanza kwenye uwanja wa michezo wa CCM
Kirumba wakati wa maadhimisho ya kilele cha sherehe za Mei mosi
zilizofanyika Kitaifa jijini Mwanza kwa mwaka huu wa mwisho wa utawala
wake.

Dkt. Kikwete aliimba wimbo wa Bendi ya OSS (Ochestra Safari Sound) wenye mashairi yasemayo “Mimi msafiri bado niko njiani sijui lini nitafika… naulizia watu kule ninakokwenda….”  na kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa dansi waliomshangilia ambapo alijiamba kuwa na sauti ya mauzo.

“Mmesikia
sauti yangu si mbaya sana,  hakika nisingekuwa Rais wa Nchi hii basi
nigekuwa msanii wa bongo fleva kama akina Ali Kiba, Diamond na wasanii
wengine wakali nikiuza album zangu kwani ningekuwa tishio  kwa
kuimba…”
alisema.

Rais
pia alimpongeza msanii maarufu nchini wa kizazi kipya mwenye mashairi
na misamiati ya maneno magumu, Mrisho Mpoto, kwa kumtaka kujibu bango la
walimu lililokuwa na ujumbe uliosomeka “Shemeji Unatuachaje??” ambapo alijibu kwa kusema kuwa “kuoa mwalimu nitabu kweli kweli haya nimesikia.”

Aliwapongeza
viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) nchini kwa
kumwalika Mpoto “Mjomba” .Mara nyingi amekuwa akitoa ujumbe mzito
kupitia fani yake ya muziki na mashairi lakini yakifikisha ujumbe bara
bara kwa wananchi katika sherehe mbalimbali za kitaifa na makongamano .

Mpekuzi blog

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.