Raia Samia Atoa Pongezi Kwa Mama Anayekumbatia Watoto,…Soma zaidi hapa

Admin Updates1 year ago6 Views

 

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pongezi kwa Mariam Mwakabungu (25), anayejitolea kukumbatia watoto njiti waliotelekezwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana.
Ujumbe huu umetumwa siku mbili tangu gazeti la Mwananchi na mitandao yake Jumapili Julai 16 kuripoti habari kuhusu Mariam na namna alivyosaidia watoto watatu waliotelekezwa na mama zao.
Samia ametuma ujumbe huo leo Jumatano, Julai 19, 2023 uliwasilishwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Brayson Kiwelu ambaye amemkabidhi Mariam kiasi cha Sh2 milioni.
Dk Kiwelu amesema ujumbe huo umetumwa na Rais Samia ambaye amekuwa mstari wa mbele katika huduma za mama na mtoto.
“Rais ametoa Sh2 milioni fedha taslim kumpatia mama huyu kwa kujitoa kwake na amewapongeza viongozi wa Wizara ya Afya na Amana kwa ubunifu huu na uthubutu mama huyu kuwa sehemu yetu,” amesema Dk Kiwelu na kuongeza;
“Rais ameshukuru sana msaada ambao mama huyu ameutoa na amewataka Watanzania kuendelea kujitoa kwa ajili ya kuhudumia wale wenye uhitaji.”
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.