Pascal Chinyele: Nitatatua shida za Wananchi Dodoma Mjini

Masama BlogSIASAKITAIFA4 months ago250 Views

Pascal Chinyele: Nitatatua shida za Wananchi Dodoma Mjini

Na Mwandishi wetu

Dodoma.

Ndg. Paschal Chinyele (Pichani ), akiwasalimia wananchi na ambaye ni mgombea wa nafasi ya ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ameendelea kujipatia uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga,Mama lishe,Vijana wa Bodaboda na Wazee katika Kata ya Madukani ambapo leo alifanya mkutano mkubwa wa kampeni huku akimwombea kura za ushindi wa Kishindo kwenye nafasi y Urais kwa Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan,Yeye mwenyewe kwa nafasi y Ubunge pamoja madiwani wa CCM.

Katika mikutano yake ya kampeni, Chinyele amepokelewa na wananchi wa kata hiyo wakiwa na shauku kubwa ya kumsikiliza ambapo ameahidi kutatua kero zinazowakabili wafanyabishara wadogo hao maarufu kama machinga, mama lishe pamoja na Boda boda ikiwa ni pamoja na kuwajengea mazingira bora ya kufanya biashara jambo lifakalopelekea kuboresha maisha ya wana Madukani na Dodoma mjini kwa ujumla.

Chinyele pia katika mkutano huo ambao ulihudhuriwa na wazee maarufu na viongozi wa Chama Cha mapinduzi kata na wilaya ya dodoma mjini ameahidi pia kuhakikisha anaboresha miundombinu,Kuhakikisha anakuwa sauti ya wananchi kuhakikisha maji safi na salama yanaptikana kwa kiwango kikubwa jimboni huko pamoja na kushirikiana na serikali katika kuboresha huduma za afya.

Aidha Chinyele amesema eneo lingine atakalohakikisha analisimamia ni kuona wafanyabiashara hao pamoja na usalama wa maeneo yao ya kufanyia bishara yanalindwa kwani amani miongoni kwao ndicho chanzo cha wao kuweza kulipa kodi na kuleta maendeleo.

Mgombea wa CCM Jimbo la Dodoma Mjini Ndg.Pascal Chinyele akiendelea kuorodhesha Kero za Wananchi wa Kata ya Madukani ambapo alifanya mkutano Mkubwa wa Kampeni Jana.

Kabla ya kumaliza mkutano wake huo ndugu Chinyele amewashukuru Wananchi wote na Wafanyabiashara hao waliohudhuria mkutano huo wa kampeni kwani wote wameahidi kumpa kura zote Dkt Samia Suluhu Hassan,Yeye na Wagombea wote wa udiwani wa CCM ifikapo tarehe 29 Oktoba 2025

#paschalchinyele #paschalchinyele #dodomamjini #oktobatunatiki #mtukazi

SOMA HIZI HAPA:

RC Rosemary Senyamue: Matokeo ya ziara ya Kidiplomasia ndani ya Jiji la Dodoma yameanza kuonekana

SIMANZI: Aliyejitosa Kuokoa Watoto Majini, Afariki Pamoja Nao

Soma Magazeti ya Leo Jumatano,17 Septemba 2025

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.