NI KWELI DIAMOND NA DAVIDO HAZIIVI TENA? BABUTALE AUANIKA UKWELI

Admin Updates10 years ago9 Views

Diamond
na Davido wana beef? Hili ni swali ambalo watu wengi bado hawajapata
jibu lake hasa baada ya wiki hii Davido kutweet maneno yaliyohisiwa kuwa
yanamlenga Diamond.
Diamond na Davido wakicheza kwa madaha
Akizungumza
kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM Ijumaa hii, meneja wa Diamond,
Babu Tale amesema Diamond na Davido sio washkaji ila wana mahusiano ya
kibiashara tu.
“Hakuna vita mimi na menejimenti ya Davido, Tunaongea,” amesema Tale.
“Hapa
ninaweza nikakuonesha meseji za mimi na Kamala ambaye ni meneja wa
Davido. Nikinukuu maneno ya Kamala kwangu ile meseji ambayo Davido
aliposti ya kwanza hakuwa anamface Diamond according to Kamala.
Akaniambia mbona ‘watanzania wameelewa vibaya’ nikamwambia ‘tuliache
hili limepita na limeshatokea hatuwezi kuwaambia bana Davido hajaongea
hivi kwa maana hii, tutafute njia nyingine ambayo Davido anaweza
akasehewa na Watanzania,” ameongeza Tale.
“Lakini
sitaki kuamini kama Davido na Diamond wana vita. Juzi Davido alikuwa
anaposti vitu vyake sio kwa sababu ya Diamond. Watanzania wote washaanza
kusema ‘oooh Davido ashaanza kumtukana Diamond’. Nikwambie kitu kimoja
Diamond hata baada ya kufanya ile video huwaga hawachati, Diamond
akimtaka Davido ataniambia mimi au atamwambia Salam au Kamala.”

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...