NAIBU Waziri wa Kilimo amesema anafahamu changamoto zilizpo kwenye sekta ya kilimo, hivyo atashirikiana na Waziri wa Kilimo kuhakikisha wanatafuta ufumbuzi wa changamoto zilizopo kwenye sekta hiyo.
Bashe ameyasema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kula kiapo mbele ya Rais Magufuli ambapo amesema kuwa anaifahamu sana sekta ya kilimo kutokana na Spika kumteua kuwa mjumbe katika kamati.
“Wanyonge katika nchi hii wako katika eneo la kilimo na anafahamu changamoto zilizopo kwenye sekta ya kilimo na sasa nitakwenda kushirikiana na viongozi wengine kutatua changamoto.
“Nitatumia kila aina ya uwezo wangu kwa kushirikiana na Waziri wa Kilimo kutafuta ufumbuzi wa changamoto za kilimo,”amesema Bashe na kuongeza sekta ya kilimo imebeba sehemu kubwa ya wananchi ambao wanategemea kilimo, hivyo lazima sekta hiyo isimamiwe vizuri.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/30S0T1h
via

