MWONE MSANII IRENE UWOYA AZUA TIMBWILI NYUMBANI KWA MUME WA MTU…NI BALAA

Admin Updates10 years ago4 Views



NYOTA
wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya amesababisha tena ! Safari
hii amekinukisha nyumbani kwa mwanaume aliyewahi kuwa mpenzi wake ( jina
tunalo) kufuatia jamaa huyo kufunga ndoa na mwanamke mwingine na
kumfanya Uwoya kuendelea kuwa ‘ nyumba ndogo ’ . Kwa mujibu wa chanzo
chetu, ishu hiyo ilichukua nafasi juzikati, nyumbani kwa mwanaume huyo,
Sinza- Mori jijini Dar es Salaam.

MCHEZO ULIVYOKUWA

Chanzo
kilidai kwamba , siku ya tukio , Uwoya akiwa na baadhi ya mastaa
wenzake ( hawakutajwa) kwenye kambi ya maandalizi ya kurekodi filamu
mjini Bagamoyo , Pwani, alipokea simu iliyomnyetishia kuwa , mpenzi wake
huyo amefunga ndoa na mwanamke mwingine jijini Mwanza , kwa hiyo yeye
aliye tu !

UWOYA ACHANGANYIKIWA

“Uwoya alipopata
salamu hizo kwa njia ya simu alichanganyikiwa ! Alianza kusema maneno ya
kumshutumu waziwazi huku akiangua kilio . Mbaya zaidi aliyemjulisha
ishu hiyo alisema ndoa hiyo ilishafungwa na si kwamba ipo kwenye
maandalizi . “Akasema anaondoka kambini kumfuata jamaa yake na kwamba
atamtambua kwani nia yake ilikuwa kwenda nyumbani kwake kumfanyia fujo
na huyo mke mpya , ” kilisema chanzo hicho cha uhakika . Nyumba
anayodaiwa kufanya fujo

AANZIA DUKANI

Chanzo
kilizidi kudai kwamba, licha ya wasanii wenzake kumsihi asichukue hatua
hiyo anaweza kuishia polisi , Uwoya hakukubali, aliondoka kwa hasira na
breki yake ya kwanza ilikuwa kwenye duka kubwa la jamaa huyo lililopo
Mikocheni , Dar ambapo alifanya fujo. “Kule alipogundua huyo mwanaume
wake hayupo ndiyo akaondoka hadi nyumbani kwake, Sinza ambako
aliendeleza fujo zake kwa kutukana na kutishia mambo mengi, ” chanzo
kilisema .

HASIRA PEMBENI

Kwa mujibu wa chanzo, ni
dhahiri kuwa , Uwoya aliondoka eneo hilo baada ya kuanza ‘ kujaza nzi ’ (
watu kuwa wengi ) ambapo aliondoka mdogomdogo na kama hana hasira
utadhani si yeye aliyekuwa akichafua hali ya hewa .

MATEGEMEO YAKE

Habari
za ndani ziliendelea kudai kuwa , Irene alishikwa na hasira za jamaa
huyo kuoa kwa vile alikuwa akiamini zali hilo lingetua kwake baada ya
ndoa yake na msakata kabumbu wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘ Katauti’
kwenda halijojo! “Uwoya alitegemea angeolewa yeye, sasa kusikia jamaa
kaoa mwanamke mwingine tena kwa siri, ilimfanya aishiwe nguvu ,”
kilisema chanzo.

ALICHOAMINI

Habari zinazidi kudai
kwamba, alichoamini Uwoya ni kwamba kitendo cha mwanaume huyo kuoa
kingemfanya yeye aendelee kuwa ‘ nyumba ndogo ’ jambo ambalo hakupenda
kulisikia hata kidogo .

UWOYA HUYU HAPA

Baada ya
gazeti hili kunyetishiwa filamu nzima, lilimsaka staa huyo na kubahatika
kukutana naye maeneo ya Sinza Palestina jijini Dar ambapo alikiri
kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba, alishaachana na mwanaume huyo.
“Ilitokea, lakini nilishaachana naye . Unajua ishu si kwamba angenioa
mimi , ila kitendo alichokifanya hakikuwa cha uungwana , ” alisema Uwoya
.

AMWANGA CHOZI

Katika hali isiyotarajiwa , msanii
huyo alianza kumwaga chozi bila kusema sababu hata pale alipoulizwa
kama chozi hilo lilitokana na kukumbuka tukio la jamaa yake kufunga ndoa
kwa siri au la! Uwoya: “We niache tu , nina mambo mengi sana
yanayoniliza mimi .” Kwa upande wake mwanaume huyo alipopatikana kwa
njia ya simu na kueleza ishu nzima alijibu kwa kifupi: “Haiwahusu .”
Kisha akakata simu.
GPL


0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Previous Post

Next Post

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.