Katika pita pita za Masama Blog Mikoa mbalimbali hasa ikimulika zaidi Viongozi wa Serikali na watendaji wake,Leo Kamera ya Masama Blog imekutana usi kwa uso na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ileje mkoani Songwe Ndugu Haji Mnasi mwenye traki suti ya bluu ambapo amekiri kusema hiyo ni desturi yake kila mwisho wa Mwezi ambapo anapenda kuwaonyesha mfano na kushirikianana Wananchi wake katika kuweka mazingira safi…

Masama Blog imefurahishwa na kitenso cha Mkurugenzi huyo kuunga mkono kwa Vitendo sheria ndogo ya kufanya usafi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi ambapo iliasisiswa na Makamu wa Rais mama Samia Suluhu Hassan cini ya Serikali ya Dkt John Pombe Magufuli yenye dhana ya Hapa Kazi tu…
Hongera Sana Haji Mnasi kwa kuwa mfano Bora.