MUONE HUYU RAPPER ALIVYOMUA MKEWE NA KUJIUA, KISA KIZIMA HIKI !!!

Admin Updates10 years ago6 Views





Rapper wa Marekani, Earl Hayes amemuua mke wake Stephanie Moseley
aliyekuwa staa kwenye kipindi cha “Hit the Floor” cha VH1 kwa risasi na
yeye kujiua kutokana na wivu wa mapenzi.

stephanie-moseley


Stephanie Moseley


Hayes alikuwa ameumizwa na uhusiano wa kimapenzi aliokuwa nao mke wake
na Trey Songz. Stephanie Moseley aliuawa nyumbani kwao na mume wake
huyo huko Los Angeles.

Hayes45


Hayes


Vyanzo vilivyo karibu Hayes, vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa Hayes
alitengana na mke wake miaka miwili iliyopita baada ya kugundua
alimsaliti na Songz. Walirudiana lakini Hayes hakuwa amepona kidonda
cha kusalitiwa na kwenye mazungumzo yao mara nyingi alikuwa
akikumbushia suala la Songz.


Trey ametweet:

R.I.P babygirl. Once an angel on earth, now watching over us from Heaven. You’ll b missed but never forgotten. Love


Hayes alimshutumu mke wake kwa kuwa pia na uhusiano na mastaa wengine.
Stephanie alikuwa dancer wa waimbaji maarufu wakiwemo Chris Brown na
Usher, japo hakuwataja kama chanzo cha mgogoro wao.

Chris-Brown-and-Stephanie-Moseley


Chris Brown na Stephanie


Hayes na Moseley walifunga ndoa mwaka 2008 na marafiki zao wanasema
alikuwa akimpenda mno mke wake. Chanzo kingine kimeuambia mtandao wa
HollywoodLife.com kuwa Hayes alikuwa anaendelea kumhisi mke wake
anamsaliti kabla ya kumuua.

Trey Songz


Kimesema Stephanie alikuwa anataka kumuacha mumewe kutokana na tabia
yake ya kumchunga muda wote. Kimeongeza kuwa rapper huyo aliwahi
kutishia kujiua kama mke wake angemuacha na kweli Stephanie alikuwa
amuache miezi miwili iliyopita.


Katika hatua nyingine, mtandao wa TMZ umedai kuwa bondia Floyd
Mayweather alikuwa akiwasiliana na Hayes aliyekuwa rafiki yake kupitia
mtandao wa video wa FaceTime na alishuhudia yote yaliyotokea.


Rapper huyo alimpigia Floyd kutumia FaceTime Jumatatu asubuhi akiwa
amekasirika kutokana na madai kuwa mke wake si mwaminifu. Kwa mujibu wa
vyanzo, Earl alisema angemuua mke wake. Bondia huyo alijitahidi
kumuomba asichukue uamuzi huo lakini alishindwa.


Floyd hajasema alichoona lakini amekubali kuwa alikuwa shuhuda na
alisikia kila kitu. Floyd yupo kwenye wakati mgumu kutokana na tukio
hilo.

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.