MSANII WASTARA ALIA NA MASTAA KUSUSIA KISOMO CHA MUMEWE SAJUKI

Admin Updates10 years ago6 Views

 
Diva wa filamu Bongo, Wastara Juma.
Na Mayasa Mariwata
DIVA wa filamu Bongo, Wastara Juma amelia na mastaa wenzake wa filamu kususia kisomo cha marehemu mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’.
Msanii
huyo mwishoni mwa wiki iliyopita aliandaa kisomo cha kumuenzi marehemu
Sajuki ambapo dua ilianzia kwenye makaburi ya Kisutu alipozikwa na
kumalizika nyumbani kwake maeneo ya Tabata Barakuda jijini Dar.
Wastara Juma akiwa katika kaburi la mumewe Sajuki.
Akipiga
stori na paparazi wetu mwanadada huyo ambaye alionekana akiangua kilio
kizito kwenye kaburi la mumewe huyo alisema, kamwe kwenye maisha yake
hataacha kumlilia Sajuki sababu ndiye mwanaume pekee aliyemuonesha
upendo wa kweli na kujivunia thamani yake kama mwanamke anayeishi kwenye
ndoa.
Kuhusu mastaa kususia kisomo hicho, Wastara alisema;
 “Hilo
nililijua mapema sababu hawa wasanii wenzangu mambo ya maana hawapendi
kabisa, hapa ungewaalika kwenye sherehe yenye pombe wangefika kwa wingi
lakini suala la dua wameona tabu sana kuja, nimeshazoea siwezi kulipa
kisasi kwa yeyote yule nitajumuika nao kama kawaida japo jambo hili
limenikwaza mno.”



Baadhi ya mastaa waliofika katika kisomo hicho ni Davina, Sandra, Vanitha, Frank, Nisha na Mtitu.

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.