- Home
-
- MSANII MAINDA AFUNGUKA:MASTAA WA BONGO WAMEJAA ZAMBI NA KUTUMIA MUDA MWINGI KUPIGA MAJUNGU.
MSANII MAINDA AFUNGUKA:MASTAA WA BONGO WAMEJAA ZAMBI NA KUTUMIA MUDA MWINGI KUPIGA MAJUNGU.
WAKATI
tukiwa tunakaribia kumaliza mwaka 2014, msanii wa filamu Ruth Suka
‘Mainda’, amedai kuwa hakuna jambo ambalo mastaa wa Bongo wamelifanya
zaidi ya kuchuma dhambi na kutumia muda mwingi kupigana majungu kuliko
kumcha Mungu kwa matendo mema.
Akizungumza na gazeti la Uwazi, Mainda alisema kuwa ndani ya tasnia ya
filamu bado mambo ni magumu kwani mastaa wengi wamekuwa nyuma na matendo
ya Mungu kwa kufanya anasa kila kukicha huku wengine wakizidi
kuchafuana kwa kupigana majungu.
“Ni kweli mwaka umeisha lakini lazima
tujue wapi tumekosea, lakini wasanii wetu hawana roho ya kuamini kuwa
Mungu yupo ndiyo maana wanapigana majungu kila kukicha.
Tangu kifo cha kipenzi Kanumba kutokea
nilisemwa sana na baadhi ya wasanii wakidai kuwa siwezi kuwika tena
lakini wanasahau kuwa niko bize na kazi ya Mungu na si kupiga majungu au
kukaa kijiweni kumsema mtu,” alisema Mainda.
0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)
Stay Informed With the Latest & Most Important News