Ilidaiwa
kwamba, baada ya Lulu kuripotiwa kupangishiwa bonge la jumba la
kifahari na milionea maarufu wa jijini Arusha lililopo maeneo ya
Mbezi-Beach jijini Dar, Wolper naye anadaiwa kujibu mapigo kwa
kupangishiwa mjengo wa maana na bwana’ke uliopo maeneo hayohayo.
Kwa
mujibu wa vyanzo vyetu ambavyo ni watu wa karibu wa mastaa hao, kwa
sasa wawili hao ni moto wa kuotea mbali kwani kila mmoja amepata bwana
mwenye ‘mpunga’ mrefu.
WOTE WANALIPA SH. MIL. 30
Ilidaiwa
kwamba, kama ilivyokuwa kwa Lulu, Wolper naye analipiwa nyumba hiyo
kiasi cha dola za Kimarekani 1,500 kwa mwezi (zaidi ya Sh. milioni 2.4)
karibia Sh. milioni 30 kwa mwaka.
CHUMBA KAMA BOUTIQUE
Habari
zilidai kwamba, kama ilivyo ya Lulu, nyumba hiyo aliyopangishiwa Wolper
ina vyumba kibao vya kulala, ukumbi wa wageni, sehemu ya kulia chakula,
mabafu, majiko n.k.
Pia nje ya nyumba hiyo kuna eneo kubwa la bustani iliyopambwa kwa maua mazuri na eneo la kutosha la maegesho ya magari.
Pamoja
na kupangishiwa mijengo hiyo ya kifahari ushuani, Lulu na Wolper
wamekuwa wakioneshana jeuri ya magari waliyonunuliwa na mabilionea hao.
MAGARI
Uchunguzi
unaonesha kuwa Lulu ana mkoko aina ya Toyota Rav4 New Model wenye
thamani ya zaidi ya Sh. milioni 30.Kwa upande wake Wolper anasukuma
ndinga aina ya Toyota Prado, nalo lina thamani ya zaidi ya Sh. milioni
30.
WATOFAUTIANA VITU VICHACHE
Habari
za ‘kiubuyu’ zinadai kwamba wawili hao wanapishana vitu vichache mno
kama vile aina ya mawigi na aina ya maisha (life style) ambapo bwana wa
Wolper amempiga ‘stop’ kuigiza lakini bado Lulu anapiga mzigo.
“Lulu
na Wolper wamelamba bingo za nguvu na bahati nzuri wanaonekana wote
kupata mabwana wasiokuwa na sifa.“Kwa mfano, Lulu pamoja na kuishi
katika maisha mazuri bado anasomeshwa na tayari ameshakamilishiwa ujenzi
wa nyumba yake ambayo juzikati alimkabidhi mama yake kama zawadi.
WOLPER AKOSWA, MAJIRANI WAFUNGUKA
Ijumaa
lilimtafuta Wolper kupitia simu yake ya mkononi lakini iliita bila
kupokelewa. Mwandishi wetu alifika mtaa anaoishi Wolper, akagonga sana
geti lakini halikufunguliwa.Hata hivyo, majirani wa staa huyo wamedai
kuwa amekuwa akionekana akiingia na kutoka akiwa ndani ya gari hilo aina
ya Toyota Prado. Jitihada za kumtafuta zinaendelea