MSANII AUNTY EZEKIEL NA WEMASEPETU WAANGUA KICHEKO MAKABURINI MCHANA KWEUPEE!!!KISA HIKI HAPAAA

Admin Updates10 years ago7 Views

Mastaa wa Bongo, Wema Sepetu na shostito wake, Aunt Ezekiel
wakiangusha kicheko katika kaburi la marehemu Albert Mangweha ‘Ngwea’.

INAWEZEKANA ilikuwa utani? Au ‘waliamka’
nazo?! Kweli binadamu anaweza kuvunjika mbavu (kicheko) juu ya kaburi la
mpendwa wake? Mh!

Lakini imetokea! Wakati dunia
ikisherehekea ujio wa mwaka mpya wa 2015, mastaa wa Bongo, Wema Sepetu
na shostito wake, Aunt Ezekiel walionesha jambo tofauti kufuatia kutinga
kwenye kaburi la aliyekuwa nyota wa Bongo Fleva, marehemu Albert
Mangweha ‘Ngwea’ na kutumia muda mwingi kucheka na kutuma meseji kwa
simu wakiwa juu ya kaburi hilo.
ENEO LA TUKIO
Tukio hilo
lililonaswa zimazima na kamera za Risasi Jumatano, lilijiri Januari
Mosi, mwaka huu kwenye kaburi la Ngwea lililopo katika Makaburi ya
Kihonda mjini Morogoro.

ILIVYOKUWA
Aunt ndiye aliyeanza
kutia timu kwenye makaburi hayo na kukaa. Baadhi ya ‘kruu’ ya Wema,
akiwemo Petit Man nayo ilifika na kuungana na Aunt.Baada ya dakika tatu,
Mama la Mama, Wema aliwasili akiwa ndani ya nguo isiyokuwa ya mtoko,
akakaa upande wa pili wa kaburi. Yeye na Aunt walikaa kwa kupeana ubavu.

CHA AJABU SASA
Awali ilidaiwa kuwa, kruu hiyo ilipanga kuwa
baada ya kufika kwenye kaburi hilo wangefanya dua fupi kwa ajili ya
kumwombea marehemu apumzike kwa amani huko aliko.Lakini cha ajabu, kabla
ya ibada hiyo, Wema, Aunt na wafuasi wao walikuwa wakipiga stori za
hapa na pale na katika hali ya kushangaza zaidi, ilifika mahali wakaanza
kucheka kile kicheko cha kuvunjika mbavu bila shuhuda wa tukio hili
kujua nini hasa kilichokuwa kikiwachekesha!

…Wakizidi kucheka katika kaburi hilo. 

Baadhi ya wapita njia waliokuwa wakikatiza karibu na makaburi hayo,
nao walipigwa na butwaa kuwaona watu hao, walioamini ni ndugu wa
marehemu, wakiangua vicheko kama hawana akili nzuri. kwa nukta kadhaa
walisimama na kushangaa kabla ya kuendelea na ‘hamsini zao’.-

WEMA ATUMIA SIMU KUFICHA USO
Ni
dhahiri kuwa, Wema alijishtukia kuwa kitendo cha kucheka juu ya kaburi
hakikuwa na ujazo wa kiungwana hivyo haraka sana aliweka simu sehemu ya
midomoni na kumfanya asionekane kwenye kamera kwamba alikuwa akicheka.
Miwani ya jua aliyovaa pia ilimsaidia.

Wakati Wema akionesha
ubinadamu huo, ‘mwenzangu na mimi’, Aunt yeye alijimalizia kiu yake ya
kicheko mpaka pale alipoamua mwenyewe kuacha na si kwa kuogopa kamera
wala malaika waliolizunguka kaburi lile (kama wapo) la mmoja wa marapa
bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania.

WEMA AJIELEZA KWA RISASI
Baada
ya wote kuacha kucheka na kila mmoja kuchukua nafasi ya ubinadamu,
paparazi wetu alimuuliza Wema ni kwa nini walionesha kuwa na furaha juu
ya kaburi la staa huyo.Wema:“Tumepita hapa ili kumuombea ndugu na rafiki
yetu Mangweha hivyo hatuna lengo lingine zaidi ya hilo.“Ishu ya kupiga
stori na kucheka, tusingeweza kuacha kuongea eti kisa tupo kaburini,
maana kila kitu lazima kijadiliwe hata kukaa hapa tumekaa kwa sababu
tunafarijika kuona kaburi la mwenzetu.”

 

Albert Mangweha ‘Ngwea’ enzi za uhai wake. 
KWA NINI WALIFANYA ZIARA KABURINI KWA NGWEA?
Awali, mastaa hao na
wapambe wao walikuwa na shoo ya kuukaribisha Mwaka Mpya iliyofanyika
Desemba 31, 2014 ndani ya Ukumbi wa Matei Lounge mjini Dodoma.Wakiwa
wanarudi Dar, walipiga kituo mjini Morogoro ambapo miongoni mwa mambo
waliyokuwa nayo kwenye ratiba ni kulitembelea kaburi la Ngwea na
kuangusha dua fupi.

Hata hivyo, baada ya yote hayo, kundi hilo
la Wema na watu wake hatimaye walifanya dua fupi ya kumuombea malazi
mema Albert Mangweha.

KUMBUKUMBU MUHIMU
Mangweha alikuwa
msanii wa Bongo Fleva. Akiwa na miaka 31 alifariki dunia, Mei 28, 2013
nchini Afrika Kusini. Chanzo cha kifo chake inadaiwa ni matumizi
yaliyopitiliza ya madawa ya kulevya. Alizikwa Morogoro, Tanzania, Juni
6, 2013.

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...