Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini Paul Ntinika akifungua Semina ya Viongozi na Watendaji wa TUGHE katika Ukumbi wa Mkapa uliopo katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya.(PICHA NA KHAMISI MUSSA)
NA KHAMISI MUSSA
“Nampongeza Rais wa Jamhuru ya Muungano wa Tanzania, Jana wakati akiwaapisha viongozi na kutoa hutuba, namshukuru sana kwa sababu amendelea kusisitiza na kutoa maagizo makali kwa wale tunao msaidia”
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Paul Ntinika leo Septemba 23, katika Ufunguzi wa Viongozi na Watendaji wa TUGHE katika Ukumbi wa Mkapa uliopo katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Aidha alisema;
“Mbeya ipo salama kabisa ikiwa chini ya Mkuu wangu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila Shupavu, Mkomavu, mfalisafa, mbobezi wa Elimu kali ambae kwa muda huu nazungumza yupo Iringa akiwa na Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa nyanda za juu Kusini wakizungumzi swala la utalii.”
“Leo Kabla sijaleta hotuba hii ya Mheshimiwa Mkuu wetu wa Mkoa Albert Chalamila kwa heshima kubwa na unyenyekevu mkubwa mimi naitwa Paul Ntinika ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya”
“Asubuhi ya leo wakati nakuja hapa nilianza na kikao na watumishi wa Halmashauri lakini nikawa naangalia kwenye mitandao tayari nikaona kabisa jina langu limebaki kuwa mkuu wa wilaya ya Mbeya, piga makofi kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”
“Nichukuwe nafasi ya kumshukuru sana lakini embu tumpongeze Mkuu wetu wa Mbeya kwa kuniruhusu mimi kuja hapa kutoa hutuba yake nimshukuru mwenyezi Mungu kwa kutujalia Afya njema na kwa uwezo wake tumeweza kukutana hapa kwa ajili ya kuendesha Semina yetu ya mafunzo kwa waajiri na viongozi wa matawi.”
“Ndugu wana Semina nichukue nafsi hii kuwapongeza Waajiri wote wa Taasisi za Umma na Binafsi ambao wamewapatia nafasi ya kujifunza na kupitia hutuba hii nikiwa namwakilisha Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wetu wa Mbeya amaye na yeye alikuwa anamwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”
“Niwaombe Waajiri wote waige mfano wa TUGHE na pamoja na vyama vingine vya Wafanyakazi kufanya semina kama ya leo inayoanza Septmba 23 na tunategemea kumlizika tarehe 27, 2019.”
“Pamoja na makongamno mbalimbli ili kupunguza migogoro mahali pa kazi pia nikushukuru Katibu Mkuu kwa maelezo mafupi kama historia inavyo jieleza kwamba vyama vya wafanya kazi ndio chachu pekee yakumkomboa mfanyakazi mahala pakazi.”
“Hivi karibuni Rais wa TUCTA wiki moja walikuwa mahali hapa walikuwa na kikao lakini kupitia vyama vya wafanyakazi, migogoro mbalimbali mfano Mkoa wetu wa Mbeya kulikuwa na wafanyakazi watano ambao walikuwa wameenda kinyume kwa fedha hizi za wajasiliamali na agizo la Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa likuwa wachukuliwe hatua kali.
Lakini kupitia vyama vya wafanyakazi walimuomba na walikuwa wamekaa ndani muda wote na mimi nilikuwa nasimamia hili kweli vyama hivi vinastahili kupongezwa wameachiwa huru na leo asbuhi nimewaona wanaendelea vizuri kwahiyo hongereni sana.”
“Ndugu wanasemina, Semina hii imejikita katika kutoa Elimu kwa waajiri pamoja n viongozi wa matawi ikiwa kama sehem mojawapo kupunguza migogoro mahala pa kazi na kwa kuzingatia sheria ya ajira na mahusiano kazini namba 6 ya mwaka 2004 na kanuni za kudumu katika Utumishi wa Umma za mwaka 2009 tukizingatia sheria hizo baina ya mwajiri na mfanyakazi tutatoa huduma sahihi kwa wananchi.”
Kutokana na huduma bora kwa wananchi tutatimiza azma ya kaulimbiu ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa John Pombe Magufuli kwamba HAPA KAZI TU
Ndugu wanasemina kupitia mafunzo mtakayo yapata kwa muda wa siku tano, tunaporudi sehemu zetu za kazi tuwe chachu kwa wafanyakazi wengine ambao tumekuja kuwakilisha kwa kuyatekeleza yale tutakayojifunza katika Semina hii
Pia nimeelezwa kuwa tuna mwezeshaji mahiri ambao () kutoka katika Utumishi wa Umma hivyo tuwatumie vizuri katika kujifunza na kuyaishi yale yote mtakayo fundishwa, Semina hii ni mwendelezo wa Semina iliyofanyika Mkoa wa Mtwara na kupata matokeo chanya ikiwemo kutoa Elimu kwa wafanyakzi ili waweze kujiunga na Chama pia Chama cha Wafanyakzi wa Serikali na Afya yaani TUGHE wamekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki na maslahi kwa wafanyakazi mahala pa kazi.
Mfano mzuri tumetoka kutoa ushirikiano madhubuti wa kupinga Kikikotoo ambacho hakikuwa na tija kwa wafanyakazi wa Umma na Sekta Binafsi kilichokuwa kinatoa maslahi madogo kwa mtumishi anapostaafu.
Jambo hili limerudisha matumaini kwa watumishi hata watumishi wa hapa Wilaya ya Mbeya wameendelea kufanya kazi sana kama msimamizi wa Serikali katika Wilaya ya Mbeya na ndio maana nataka niseme
Wakati Mwenge wa uhuru unapita katika Wilaya tumesimamia shughuli zote za maendeleo

Mwenyekiti Kamati ya Wanawake Tawi la TUGHE MOI na Afisa Muuguzi wa Taasisi hiyo Georgina Chirwa (kushoto) akisalimiana na Afisa Elimu Chama cha TUGHE Nsubisi Mwasandende wakati wa Semina iliyoandaliwa na Chama hicho katika katika Ukumbi wa Mkapa uliopo Mkoa wa Mbeya
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bi Tabu Mambo akitoa utambulisho mfupi kwa baadhi ya viongozi
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Tabu Mambo (kulia) akisikiliza kwa umakini wakati mgeni rasmi alipokuwa akizungumza na wana semina hiyo iliyoandaliwa na TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam.kushoto ni Katibu TUGHE Mkoa Morogoro Sara Rwezaula na Katibu wa Mkoa TUGHE Mkoa wa Temeke Dar es Slaam
Baadhi ya wajumbe wakifuatili kwa umakini wakati Mkuu wa Wilaya Paul Ntinika (pichani hayupo) alipokuwa akifungua Semina hiyo iliyoandaliwa na TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam
Baadhi ya washiriki wa Semina hiyo wakifuatilia kwa umakini wakati Mkuu wa Wilaya Paul Ntinika (pichani hayupo) alipokuwa akifungua Semina hiyo iliyoandaliwa na TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa Mkapa uliopo Mkoa wa Mbeya leo Septemba 23. 2019.
Mjumbe Kamati ya Utendaji ya Dar es Salaam na Dkt. Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Peter Kibacha (kulia) akiwa na baadhi ya viongozi katika Semina hiyo. kuanzia kushoto ni Katibu TUGHE Mkoa wa Songwe Mwanaidi Mgowa, Katibu TUGHE Mkoa wa Mwanza Amini Msambwa na Mwenyekiti wa Semina Ibrahim Nuru Mmbaga.
Taswira ya Ukumbi
Mwenyekiti TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Mziwanda Chimwege akizungumza jambo katika Semina iliyoandaliwa na TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam leo Septemba 23, 2019 katika Ukumbi wa Mkapa uliopo Sokomatola Kata ya Maendeleo Mkoa wa Mbeya
Mwenyekiti wa Semina Ibrahim Mmbaga akifafanua jambo katika Semina hiyo
Baadhi ya viongozi mahala pa kazi wakimsikiliza Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Paul Ntinika wakati akifungua Semina ya Kamati tendaji leo Septemba 23 katika Ukumbi wa Mkapa uliopo katika Mkoa huo wa Mbeya
![]() |
| Mdhamini wa TUGHE Dkt. Yonah Mabela (kulia) akizungumza jambo na baadhi ya viongozi kabla ya Semina kuanza nje ya Ukumbi wa Mkapa uliopo katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya. kuanzia kulia ni Mwenyekiti TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Mziwanda Chimwege akizungumza na Mwenyekiti wa Semina Ibrahim Mmbaga akifafanua jambo katika Semina hiyo
|
Mwenyekiti wa Semina Ibrahim Mmbaga akifafanua jambo katika Semina hiyo akizungumza jambo na waandishi (hawapo pichani) wakati wa Semina ya Viongozi na Watendaji wa TUGHE katika Ukumbi wa Mkapa uliopo katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bi Tabu Mambo (wa katikati) akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Paul Ntinika na kulia ni Naibu Kkatibu Mkuu TUGHE Jane Mbura
Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa Henry Mkundi akizungumza katika Semina ya Viongozi na Watendaji wa TUGHE katika Ukumbi wa Mkapa uliopo katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya alianza kwa kumshukuru Mheshimiwa Rais ambaye ni msikivu anaye penda kutetea wanyonge ni kwa kuweza kusikiliza kilio cha wafanyakazi na kulifanyia kazi ombi lao kwa kuruhusu Kikokotoo cha awali kiendelee kutumika kwa muda maalum wakati utaratibu shirikishi zaidi ukiandaliwa alisema; Mkundi
Mgeni rasmi akizungumza na washiriki wa Semina hiyo iliyoandaliwa na TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam.
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na wajumbe na baadhi ya wawakilishi wa waajiri
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na wajumbe katika Semina hiyo
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozo
from CCM Blog https://ift.tt/2mGkRNL
via






















