Mc Pilipili Afunguka Sababu ya Kumwaga Chozi Wakati wa Kumvalisha Pete Mchumba Wake

Special Correspondent6 years ago5 Views

Mc Pilipili Afunguka Sababu ya Kumwaga Chozi Wakati wa Kumvalisha Pete Mchumba Wake

Baada ya hivi karibuni mchekeshaji maarufu Bongo, Emmanuel Mathias ‘MC Pilipili’ kumvisha pete ya uchumba, mchumba’ke, Philomena Thadei na kuangua kilio, mwenyewe ameibuka na kufichua kilichomliza.

MC Pilipili aliangua kilio cha aina yake wakati akimvisha pete mrembo huyo na kuzua gumzo la aina yake kwani imezoeleka kwenye zoezi kama hilo mara nyingi wanawake ndiyo huwa wanaangua vilio.

Kutokana na gumzo hilo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta MC Pilipili na kumuuliza kuhusiana na kuangua kwake kilio ambapo alieleza kuwa alilia kutokana na changamoto alizokuwa amezipitia kwenye masuala ya uhusiano wa kimapenzi na msichana huyo.

Alisema hadi kufikia hatua hiyo ya kumvisha pete na binti huyo kukubali, halikuwa jambo rahisi bali alikumbana na ugumu hivyo alipoyakumbuka hayo, alijikuta machozi yakimtoka.

“Nimepata misukosuko mingi sana kwenye uhusiano ndiyo maana hadi machozi yamenitoka kwa furaha kwa kuwa nimefikia hatua nzuri, natarajia kuanza vikao vya maandalizi ya harusi hivi karibuni na vitakuwa vya muda mchache kwa kuwa ninataka kufanya haraka iwezekanavyo,” alisema MC Pilipili.

Kwa upande mwingine MC Pilipili alisema kuwa, ndoa yake itakayofanyika hivi karibuni inatarajiwa kuhudhuriwa na wageni waalikwa 2,000 ambapo wachekeshaji watakuwa ndiyo washehereshaji huku ikihudhuriwa na viongozi mbalimbali hivyo itakuwa ni harusi ya aina yake

from UDAKU SPECIAL BLOG http://bit.ly/2Fh48IT
via

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.