MAPENZI:SHOGA KATIKA MAHUSIANO YAKO USITAFUTE MCHAWI, UMEJIROGA MWENYEWE..SOMA HAPA UELEWE

Admin Updates10 years ago5 Views

Jamani
hamjambo? naona viroho vinawadunda baada ya kuufunua ukurasa huu na
kujiuliza leo kombora linaangukia kwa nani? Narudia, sipo kwa ajili ya
kuwarusha roho bali mtajirusha wenyewe kutokana na tabia zenu mbaya.
 Nia yangu ni kumuona mwanamke mwenzangu mambo ya kike hayampiti kando.
Jamani
kuna mambo mengine yanasikitisha, hivi kwa nini umuogope mwanamke
mwenzio mwenye viungo kama wewe. Wiki iliyokwisha nilielezea makosa ya
nyuki kukimbia mzinga wake kwa sababu tu mtu katia mkono na kulamba
asali yako.


Ukiona
mtu katia mkono kwenye mzinga wako ujue asali yako ni  tamu unatakiwa
kuilinda na siyo kuukimbia mzinga kuwaruhusu watu wajilambie kwa raha
zao, haipendezi. Hizo ni hasira za mkizi na kutoa kafara kwa mvuvi.
Nimeliongelea hili kwa vile makavu ya leo yanafanana na hilo.


Juzi
nilikutana na mtoto wa shoga yangu akiwa anatoka sokoni, katika
mazungumzo yetu si unajua mimi mtu wa utani. Sijui kukasirika kijinga,
 mtoto wa kike niliumbwa siku Mungu akitabasamu nami nikawa na umbile la
tabasamu, siyo wewe uliumbwa Mungu amechoka kila wakati uso kama ndimu
,unacheka hujulikani, umenuna hujulikani!


Si
kwamba nazungumzia wenye sura mbaya, bali wenye sura zilizokosa
tabasamu, siwezi kumhukumu mtu kwa maumbile kwa vile mimi sijawahi
kuumba. Ila nazungumza na tabia za watu, Mungu kawaumba na sura nzuri
lakini imeharibika kwa kukunja uso na kupinda midomo.


Hebu
tuachane na hayo tuendelee na yetu, basi katika kutaniana si ndiyo
aliponieleza kaamua kurudi kwao baada ya mumewe kuoa mwanamke mwingine.
Nilimuuliza kipi kikubwa kilichomuondoa kwa mumewe ikiwa dini yake
inamruhusu. Alinijibu jibu la kitoto ambalo lipo katika vichwa vya
wanawake wengi.


Eti
ameondoka kwa vile hawezi kushea mwanaume na mwanamke mwenzake. Jibu
lake lilinifanya nimwangalie chini mpaka juu hadi akashtuka na kuniuliza
kulikoni kumuangalia vile.  Nilichomueleza nataka nikae na wewe chini
nikueleze uache ujinga wa kijinga!


Jamani
 ni kweli wanawake tupo kama mdudu wa sikio tusiotaka mshirika, lakini
kutokana na hali ya sasa hivi kuwa na wako wa peke yako ni kazi.
Afadhali dini nyingine zinaruhusu mpaka wake wanne, lakini dini
zilizokataa tunaona jinsi gani viongozi wao wanavyoingia kwenye kashfa
ya kuwa na wanawake wengi tofauti na muongozo wa dini yake.


Siyo
kwamba nahalalisha lakini ukweli ndiyo ulivyo asilimia kubwa ya nyumba,
waume zetu wana wanawake zaidi ya mmoja. Wengine tunawakamata na
wasichana wetu wa kazi, imefikia hata kuwapa ujauzito.


Hii
yote inatokana pengine na udhaifu wetu ndani ya ndoa kwani wengi baada
ya kuolewa hujisahau na kuamini ukishaolewa umemaliza.Tumekuwa
hatuzithamini ndoa zetu kwa kuamini baada ya kuolewa hakuna kingine
zaidi kwa mumeo kama umemvulia nguo ya ndani ndiyo baaaasi. Tunasahau
mwanaume unatakiwa kumtunza kama mtoto kwani wewe ndiye kila kitu kwake,
siyo kasoro zitolewe na mwanamke wa pembeni.


Pengine
mumeo hakuwa na wazo la kuongeza mwanamke mwingine, lakini mwenzako
aliona mapungufu yako na  kuyafanyia kazi ndiyo yakamfanya mumeo aingie
kichwakichwa baada ya kunasa, aliendelea kumpa vitu adimu ambavyo kwako
hapati. Ili afaidi vizuri anamuoa kabisa ili asile kwa kujificha.


Unaletewa
mke mwenza unakimbia kumbe sababu ni wewe. Kaingia ndani hutakiwi
kukimbia, jirekebishe pigana  kuhakikisha unairudisha namba moja yako.


Nina imani nimesomeka vizuri, basi kwa leo inatosha tukutane wiki ijayo, ni mimi Anti Nasra, Shangingi Mstaafu.

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.