MAPENZI:NIMEVUMILIA NIMECHOKA BORA NIWE MKWELI…MPENZI KANIKIMBIA NA MTOTO WANGU,NAOMBA USHAURI

Admin Updates9 years ago5 Views

Kuna Vitu Ambavyo Unaweza Kukutana Navyo Katika Maisha Yako ya Kila Siku na Ukavihifadhi Katika Moyo Wako Na Kufanya Siri Kubwa Ambayo Kamwe Hutataka Kumwambia Mtu Yoyote Yule. Katika Maisha Ambayo Nimeishi Hapo Kabla ikiwa Bado Sijakutana na Huyu Mpenzi Niliyenae Sasa Nilibahatika Kuzaa Na Msichana Mmoja Aitwaye Sheila. Alikuwa Ni Msichana Ambaye Nilikutana nae Kibahati Mbaya Sana, Nasema Kibahati Mbaya Sana Kwa Kuwa Mazingira Tuliokutana Yalikuwa ni Mazingira Ya Msaada Zaidi Baada Ya Kumkuta Maeneo Ya Posta Mpya Saa Tano Za Usiku Akiwa Amejiinamia. Sikujua Nikitu Gani Ambacho Kilinisogeza Pale Lakini Nilijikuta Tayari Nikiwa Mbele Yake Huku Nikionyesha Roho Ya Ubinadamu Ikiwa ni Pamoja na Kuuliza ni lipi Tatizo Ambalo Linamsibu. Binti Yule Hakutaka Kunijibu Wala Kunisikiliza Alichokuwa Anakifanya Ilikuwa ni Kunitazama tu na Kunibinulia Mdomo Kwa Dharau Kubwa. Kusema Kweli binti Alikuwa ni Mrembo Sana na Alikuwa Anavutia Sana.. Kijana Nikaona nitangaze Msaada Huku Moyoni Nikiwa na Mipango Yangu Mingine. Kweli Baada Ya Vuta Nikuvute Binti Akakubali Kuondoka na Mimi Kuelekea Kigamboni Ninakoishi Huku Akiweka Angalizo La Kutokumsumbua Tukifika Huko. Mdomoni Nikakubali Lakini Moyoni Nilikuwa Mbali Sana…. Kifupi Siku Hiyo Hiyo Ndio Siku Ambayo tulifungua Ukurasa Wa Penzi Letu Na Tukawa Kama Kumbikumbi Kila Wakati tuko Wote Huku nikiwa Sijui Chochote Kuhusu Alikotoka na Kwa Wazazi Wa Huyu Mwenzangu.

Ndani Ya Kipindi Cha Uhusiano Wote mwenzangu Akapata Ujauzito Ambao Kila Mmoja Aliufurahia Sana Huku Mapenzi Yetu Yakiongezeka Maradufu. Sasa Kilichonifanya Kuja Hapa Kwenu Wanajamvi Wenzangu Ni Kwamba Licha Ya Kumhudumia Kwa Kila Kitu Kama Mwenza Wangu Lakini Baada Ya Kujifungua Binti Akanambia Alichokuwa Anakitaka Ameshakipata Hivyo Nisimjue na Nisimfuatilie Tena…. Mwanzo Niliona Ni Kama Utani Lakini Baada Ya Siku Chache Akatoroka na Mtoto Mimi Nikiwa Kazini na Hata Niliporudi na Kuwauliza Majirani Hawakuwa na Jibu La Maana. Na Hata Namba Zake Za Simu Kila Nikipiga Hazipatikani Tena Lakini kuna Siku NIlitumiwa Sms Kwa Namba Ngeni Akinipa Hongera Ya Kumpatia Mtoto… Lakini Nilipoipiga Haikupatikana na Mpaka Leo Haipatikani….. Ombi langu Kwenu Wanajamvi Wenzangu Nifanyeje Niweze Kuipata Damu Yangu? Imefikia Kipindi Nahitaji Kumuona Mwanangu Lakini Sijui Wapi Nitampata Huyu Mwanamke.

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.