MAPENZI:HAJUI KAMA NIMEOA, PENZI LIMENOGA NATAKA KUSEMA UKWELI LAKINI SUJUI NIANZIE WAPI??NINAOMBA USHAURI

Admin Updates10 years ago6 Views


Sijawahi kuwa mzinzi tangu nimeoa miaka 5 iliyopita. Hadi hivi karibuni nilipoanzisha uhusiano na binti mmoja..

Tulifahamiana kikazi, yeye yupo idara ya uhasibu. Huja kazini kwangu kila mwisho wa mwezi kwa ajili ya transaction mbalimbali.

Tukazoeana na kuwa wapenzi. Kiukweli mambo yalienda haraka haraka sana
na aliingia mazima mazima kiasi kwamba hata kila nilipotaka kumwambia
ukweli najikuta nashindwa maana alikua resi ile mbaya.

Ikawa ni mahaba niue, kila tukitoka kazini tupo wote sehemu, weekend
tutaenda cinema, beach etc. Yaani ghafla bin vuu anaongelea ndoa. Kila
siku ya Mungu lazima agusie ndoa itakua vipi.

Wakati mwingine anaingia Google kusearch magauni ya harusi na viatu na
maids wake watavaa nini siku hiyo. yaani nabaki mdomo wazi maana moyoni
najua nimeshaoa siku nyingi.

Kila akianzisha hizo story za magauni najitutumua sasa nianze
kumwelewesha kwamba nimeoa basi hunikata kauli haraka na kuendelea
kusema mambo ya ndoa yetu kwamba napendelea ukumbi gani ndo mzuri.

Sasa tuna miezi miwili ameanza kuongelea suala la kupata mtoto
ananiuliza kuwa naonaje akibeba mimba kabisa tufunge ndoa wakati ana
mimba. Basi humjibu kuwa tusubiri kwanza asibebe kabisa mimba, nikijibu
hivyo anakua mkali anauliza “hiyo mimba unaibeba wewe au mimi?” Mimi
nabaki kimya.


Kwa kweli namuonea huruma kwa mawazo aliyonayo, mimi niliingia kwenye
huu uhusiano kubadilisha mboga tu and I thought it would be a temporary
thing. Kiuchumi yupo vizuri balaa simpati hata kwa dawa.
Ukifika alipopanga thamani za vitu alizonazo ndani ni za gharama sana,
na nyumba ni ya kisasa, ana miradi mingi mbali na kazi na alinipeleka
anapojenga nyuma ni kama imeisha bado ukuta tu wa nje.

Tatizo pekee ninaloliona ni kuwa huyu binti time is ticking very fast
against her age, yupo kwenye mid 30s; somewhere between 30-36 years.
Hivyo anadhani amechelewa.

Anasema amepoteza muda mwingi kwenye relationship iliyopita iliyochukua 7
years na jamaa akaoa mtu mwingine na kumuacha yeye, hivyo anasema
hataki tena long relationship. Ameshaniunganisha na ndugu kibao. Kila
wiki natambulishwa kwa ndugu mpya.

Wakuu, naona huruma Kubreak hii news kuwa nilishaoa. Ingawa nampenda
moyoni lakini pia nimechoka maisha ya digi digi ninayoishi maana nikiwa
home kwangu usiku lazima anipigie simu na anaongea zaidi ya nusu saa na
hapo tumetoka kuonana jioni. Basi najifanya naenda dukani kwa mangi
kununua kitu na kupiga stori ili wife asishtuke kuwa naenda kuongea na
simu.

I think wengi mnajua maisha ya Ku,cheat yalivyo magumu ni utumwa, ni jela ya nje.

Wakuu nianzeje kumwambia ukweli anielewe? Au nitume mtu mwingine ndo amwambie kama anampa umbea vile?

I need to get out of this mess maana wife somehow ameanza kushtukia mwenendo wangu.

Please, advise

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.