MAPENZI: FAHAMU HAPA JINSI YA KUMTAMBUA MPENZI ALIYEKUSALITI MUDA MFUPI ULIOPITA

Admin Updates10 years ago5 Views

KUNA
BAADHI YA WATU WANAYATENDEA HAKI MAPENZI; WAPO MAKINI KWA KILA KITU
KATIKA UHUSIANO WAONA HIVYO KUWA KAMA WANAISHI KWENYE PARADISO YA PEKEE.
PIA, WAPO WENGINE AMBAO WANAYAONA MAPENZI MACHUNGU, WANAYACHUKIA
NA KWA HAKIKA WANALAANI KUKUTANA NA WENZI WALIONAO.Kwa nini? Kwa sababu
kila siku ni ugomvi, hawana amani. Hawapati muda wa kukaa na kupanga
mambo yao, kila wakikutana ni ugomvi. Kunyang’anyana simu na kupekua
meseji ndiyo sehemu ya uhusiano wao.Utakapoona wapenzi hawaishi ugomvi,
ujue kwamba wanaishi kwa mashaka. Kila mmoja haamini kama mwenzake siyo
kicheche. Pamoja na ugomvi wao, wengi wanashindwa kuwatambua wenzi ambao
wamewasaliti muda mfupi uliopita.


Katika mada yetu ya leo, tutaangalia mambo 10 ya msingi ambayo yanaweza
kukusaidia kumtambua mpenzi aliyekusaliti muda mfupi uliopita. Hapa
namaanisha utaweza kumtambua mpenzi aliyekusaliti ndani ya saa 24.

Tafadhali weka mawazo yako hapa ili uweze kumgundua mwenzi ambaye ni mwizi wa haki yako. Sasa hebu twende tukaone.

RATIBA YA GHAFLA

Rafiki zangu, ukishaanza kuwa na wasiwasi na mpenzi wako kwamba huenda
anataka kukusaliti, jambo la kwanza kabisa unalotakiwa kukumbuka ni
sehemu aliyokuambia amepitia/anakwenda kama ilikuwa katika mipango yake
au amefanya safari ya kushtukiza.


Hii ni dalili ya kwanza kabla hata hamjakutana nyumbani; “Sorry baby,
kuna sehemu napitia mara moja, nitachelewa kidogo kurudi nyumbani,”
kauli kama hii iangalie sana.


Mwingine anaweza kupiga simu na kusema: “Mume wangu, bosi ametupa ofa
ya dina wafanyakazi wote, kwa hiyo nitachelewa kurudi nyumbani, samahani
sana dear.”


Kauli hizo mbili ni alama ya kwanza katika kushibisha hoja yako ya
kusalitiwa kama ni kweli atakuwa amefanya hivyo. Kumbuka kwamba, si
lazima kila anayesema amepata dharura amesaliti.

ANAKWEPA KUWASILIANA

Mtu huyo ambaye ameshatoa taarifa kwamba amepata dharura, utashangaa
hataki kuwasiliana na wewe. Pengine ukimpigia simu, anaweza asipokee na
kama akipokea anaweza kukujibu: “Nitakupigia baadaye, samahani sipo
sehemu nzuri.”


Unaweza kumwandikia meseji lakini pia asijibu. Wapo wengine vichwa
ngumu zaidi, ambao wao kuacha kupokea simu na kujibu meseji si vitu
muhimu sana, wanazima kabisa! Ukiona dalili hii, basi ujue unasalitiwa.

UCHANGAMFU KUPITILIZA

Pamoja na mambo hayo hapo juu, lakini mwenzi huyu akirejea nyumbani,
huwa mchangamfu kupitiliza. Ana maneno mengi, anaanzisha mijadala ya
ghafla na kuifunga mwenyewe. Atajifanya anataka kufanya mambo mengi kwa
ajili yako.


Ahadi zake zinakuwa nyingi za ghafla na nyingi zipo wazi kabisa kwamba
si rahisi kuzitekeleza. Alama hii ni kati ya zile 10 zinathibitisha
kwamba ndani ya saa 24 umeibiwa mali yako.

UPOLE KUPITILIZA

Kinyume cha uchangamfu ni upole, kama mwenzi wako ametoka kimapenzi na
patina mwingine kwa ile hofu yake moyoni, anaweza kuwa mpole kupitiliza.
Anafanya hivyo kwa lengo la kutafuta huruma.


Hana sababu ya kuwa mpole, lakini anaweza kutumia ngao hiyo, ili
maswali utakayomuuliza yawe kuhusu upole na ukimya wake, usahau mambo ya
kuhisi kuwa umesalitiwa. Hata hivyo, majibu yake yanaweza kuwa ya mkato
sana: “Sijisikii vizuri, siku yangu haikuwa nzuri kabisa leo. Kuna mtu
nimetibuana naye ofisini, amenichanganya kabisa.”


Alama hii ni moja ya sababu zitakazokufanya uendelee kumchunguza katika
hatua zinazofuata ili mwisho ugundue kuwa umesalitiwa au ni wasiwasi
wako tu.

UGONJWA WA GHAFLA

Katika kukwepa usumbufu wa maswali mengi, mwingine huamua kujifanya
anaumwa. Atarudi akiwa mkimya kuliko kawaida, ukimwuliza atakujibu kuwa
anaumwa. Kama mpenzi wake, anajua wazi kuwa hutakuwa na muda wa kuanza
kuhisi usaliti badala yake utamjali na kuuliza hali yake.


Mgonjwa huyu kwa kawaida huwa haumwi magonjwa siriasi, sana sana
atakuambia hajisikii vizuri, kichwa kinamgonga au moyo unaenda mbio.
Ukizungumza kuhusu suala la hospitali atakataa akidai hana hali mbaya
sana. Mara nyingi hupenda kukimbilia kitandani, akitaka kupumzika.


Anafanya hivyo kwa sababu anakwepa aibu ya kukutanisha uso wake na
wako. Ukitaka kwenda kumnunulia dawa za maumivu atakujibu: “Nimeshameza
panadol baby.” Mwenzi wa aina hii unatakiwa umtilie mashaka, maana
inawezekana ametoka kufanya kitu kibaya.

MAJIBU TATA

Mpenzi ambaye ametoka kukusaliti huwa hapendi kuulizwa maswali mengi,
ukimwuliza majibu yake huwa tatanishi sana. Kwa kuwa ameshasingizia
kwamba anaumwa, hivyo atafika na kulala moja kwa moja.


Ukitaka kujua zaidi kuhusu kuugua kwake au dharura aliyoipata
iliyosababisha achelewe kurudi nyumbani, hukosa majibu yanayoeleweka.
Wakati mwingine anaweza kujisahau na kukupa jibu ambalo linapingana na
maelezo yake ya awali. Ukiona hivyo ujue kuna namna.

HATAKI FARAGHA

Kwa kuwa tayari ameshatoka kwa mtu mwingine, huhofia sana kukutana na
wewe faragha. Kama tulivyoona katika vipengele vilivyopita, hutengeneza
mazingira ya kukufanya msikutane kimwili, hofu yake ikiwa ni kukuficha
usigundue mchezo wake mchafu.


Kisingizio cha kuumwa, bila shaka ni kikubwa na kitakufanya ushindwe
kuwa na mhemko wa kimahaba, lakini kurudi nyumbani akiwa amekunja ndita
au mpole kupitiliza, tafsiri yake ni wewe kuogopa au kuhamisha hisia
zako kutoka kwenye mapenzi na kuanza kumfikiria yeye kama yeye.


Kwa vyovyote vile, kama ni mwenzi wako wa muda mrefu, zipo alama nyingi
zitakazoweza kukufanya ujue kuwa ametoka nje, kwanza ni vyema
kumkazania kukutana naye faragha. Hata kama atasingizia anaumwa,
ng’ang’ania kukutana naye, maana hapa ndipo penye ukweli mkubwa zaidi.


Mchunguze anavyokupokea, halafu pima uwajibikaji wake. Huwa mvivu na
asiyetaka kutoa ushirikiano. Anaweza kuishia kulalamika kuwa hajisikii
vizuri na kusisitiza mhairishe zoezi hilo.


Mpenzi msomaji, njia unayopita kila siku unaijua. Sehemu yenye
makorongo unaifahamu, yenye matuta pia utatambua, hata yenye makorongo
yenye maji yaliyosimama pia unaijua vyema, sasa ukikutana na tofauti
yoyote katika barabara unayoitumia siku zote, maana yake tingatinga
limepita.

ANAKWEPA KUSOGELEWA
Akifika tu nyumbani, atahakikisha hupati nafasi ya kuwa naye karibu. Hataki kabisa kusogelewa. Hapo anakimbia vitu vitatu;
Kwanza kabisa, inawezekana huko alipotoka alitumia manukato tofauti na aliyotoka nayo nyumbani asubuhi.

Pili, manukato ya sabuni mpya aliyotumia, anaogopa usiyasikie, tatu,
kila mtu ana harufu yake, unapokaa na mtu kwa ukaribu hasa faragha kwa
saa mbili au zaidi, kila mmoja huhama na harufu ya mwenzake.


Kwa kuwa wewe unaitambua vyema harufu ya mpenzi wako, atahofia
kukusogelea maana utashtukia. Mwisho kabisa, hata kama atakuwa amekwepa
yote hayo, labda hajaoga, hajatumia manukato mengine, bado utaweza
kumkamata kwa harufu ya manukato, sabuni au mafuta aliyotumia mtu
aliyekuwa naye.


Kukwepa kukusogelea, tafsiri yake ni kwamba hataki usikie harufu ya
tofauti kutoka kwake, maana anajua alichokifanya. Jiulize, kama kila
siku huwa mnapokeana kwa mabusu na kukumbatiana, kwanini safari hii
anakukwepa?

ANAKIMBILIA BAFUNI

Akifanikiwa kukuzuga katika kipengele kilichopita, basi safari yake
huishia bafuni. Ataenda haraka na hatataka kwenda na wewe maana kuna
kitu anajaribu kukuficha. Wengi wanaamini (kuna ukweli kwa asilimia
chache) baada ya kuoga wanaweza kupoteza ushahidi wa kutoka nje ya
ndoa/wapenzi wao.


Utakapomruhusu aoge, kwanza atatumia sabuni ya siku zote, ambayo
anaweza kuitumia kwa wingi awezavyo ili kuficha ushahidi. Atajisafisha
zaidi nyeti zake ili usijue kilichotokea muda mfupi.


Akitoka bafuni lazima atakimbilia kwenye meza ya kujipambia kisha hapo
atajimiminia manukato ili kuzima kabisa ushahidi ambao ungeweza
kumuumbua. Jiulize, kama kila siku huwa mnaoga pamoja, kwanini amekuja
ghafla na kukimbilia bafuni bila wewe?

WASIWASI MWINGI

Atakuwa mwenye wasiwasi mwingi sana, hata kama akikubali kukutana na
wewe faragha, ushirikiano huwa hafifu. Mwoga kupitiliza na muda wote
huwa anahisi kwamba hatakufikisha salama safari yako.


Wasiwasi wake hauishii hapo, hata kupeana mikono tu na kukutanisha
macho, kutakuonesha jinsi alivyo na wasiwasi. Si kama anapenda hali
hiyo, ila anazidiwa na hisia za usaliti kwa kuwa anajua alichokifanya
muda mfupi uliopita.


Kama utavifuatilia vipengele hivyo kwa makini, ni rahisi sana kumkamata
mwizi wako. Acha papara, chunguza taratibu, ukiona angalau kuna nusu ya
hizi nili zokupa hapo juu, ujue wazi kuwa unaibiwa tu

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.