
Maofisa wa Idara ya Ujasusi nchini Kenya wanaelekea Dubai ili kuchukuwa taarifa ya mwakilishi wa Umoja wa Falme za Kiarabu kuhusiana na sakata la dhahabu bandia linalochunguzwa.
Wakati huohuo, pirikapirika zinaripotiwa Bungeni za kusaka saini ili kumtimua Waziri wa Usalama wa Taifa, Fred Matiangi, kwa madai ya kuwalinda watuhumiwa wa kashfa hiyo.
Jeshi la Polisi la nchini humo linawashikilia maofisa Polisi waliokuwepo kwenye eneo ilikopatikana dhahabu hiyo bandia wakiwa wanawalinda wanadiplomasia na wala sio wahalifu.
Maofisa wa Idara ya Ujasusi walitazamiwa kusafiri jioni ya leo Jumanne (21 Mei) kuelekea Dubai ili kuchukuwa taarifa ya mwakilishi wa Umoja wa Falme za Kiarabu kuhusu sakata hilo la dhahabu bandia linalochunguzwa.
Majasusi hao walitazamiwa kumhoji Ali Zandi anayemuwakilisha Sheikh Mohammed Bin Rashid Al Maktoum na kampuni ya Zlivia inayofanya biashara ya dhahabu Dubai.
from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2HHSgPb
via
