MANENO YA WEMA SEPETU BAADA YA KUTUHUMIWA KUTOKA KIMAPENZI NA MUME WA LINAH

Admin Updates9 years ago5 Views


Siku chache baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Esterlina Sanga ‘Linah’ kulalamika juu ya kitendo cha Wema Sepetu kumchukua aliyekuwa bwana’ake Nangari Kombo, muigizaji huyo ameibuka na kutoa maneno yanayoashiria kejeli, kuwa aache presha, kwani zile ni picha tu!

Wiki iliyopita zilisambaa  picha  mtandaoni zikimuonyesha Wema Sepetu akiwa amepozi kitandani na kijana huyo, aliyepata umaarufu baada ya kuingia ndani ya eneo la kuchezea katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam mwaka 2010, wakati wa mechi kati ya Brazil na Taifa Stars na kumkumbatia kiungo nyota wa mabingwa hao wa zamani wa dunia, Kaka.
  
Katika  maelezo yake  kuhusiana  na  kusambaa  kwa  picha hizo, Wema amesema kupiga picha na Nangari hakumaanishi mapenzi, kwani yeye ni mtu wa watu na picha kama hizo hupiga na marafiki zake wengi tu, hivyo Linah asiwe na shaka naye hata kidogo.

“Nilipiga naye kama ninavyoweza kupiga na marafiki wengine kama akina Martin Kadinda, Petit Man na wengineo. Sina uhusiano naye wa kimapenzi, naomba aamini kuwa ni rafiki tu wa kawaida,” alisema Wema na kuibua maswali juu ya aina ya uswahiba wa kawaida wa kupiga picha kitandani na mpenzi wa mtu!

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.