Mahakama Kuu ya Kenya Yamzuia Ruto Kujenga Kanisa
KAMA Kuu nchini Kenya imetoa agizo la muda ya kuzuia ujenzi wa Kanisa au majengo yoyote yenye mafungamano ya dini ndani ya viunga vya Ikulu ya Nairobi, hatua inayokuja baada ya makundi manne ya kiraia kufungua pingamizi wakidai kuwa ujenzi wa jengo la kidini katika eneo la taasisi ya taifa ni kinyume cha sheria na kanuni za utawala bora.
Uamuzi huo umetolewa na Jaji wa Mahakama Kuu, Chacha Mwita ambaye amesema ujenzi huo usitishwe kwa muda hadi pale hukumu ya mwisho itakapotolewa mwezi Novemba 2025 hatua ambayo ni kama ushindi wa muda kwa wanaharakati wa kiraia, huku ukiweka shinikizo jipya kwa serikali kueleza iwapo hatua hiyo inaheshimu misingi ya kikatiba na usawa wa kidini nchini Kenya.
Hivi karibuni Rais wa Nchi hiyo William Ruto alinukuliwa hadharani akisema ameagiza kujengwa kwa Kanisa hilo kwa kutumia fedha zake binafsi, jambo lililozua mijadala mikubwa miongoni mwa wananchi na wadau wa kisheria huku wakosoaji wakisema hata kama fedha ni za binafsi, ujenzi ndani ya lkulu unaweza kufupisha mipaka kati ya dola na dini na hivyo kuibua mgongano wa kikatiba.
SOMA HIZI:
Unahitaji Ushinde Zabuni?Je Unakwama wapi?Soma HAPA
Mgombea wa CCM Ruangwa aandika haya Kuelekea uzinduzi wa Kampeni za CCM Kitaifa
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






