LIVE HII..KWANII..?WEMA NA AUNTY HUSAGANA? WADENDEKA LAIVU… DIAMOND AKASIRIKA AONDOKA..HEBU WAONE HAPA

Admin Updates10 years ago5 Views


Stori: Musa Mateja na Imelda Mtema
Ni
sheedah! Pamoja na kukanusha kwa kutumia nguvu kubwa, nyuma ya ushosti
wa mastaa grade one wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu ‘Gorgeous Onyinye’
na Aunty Ezekiel kuna siri nzito ikidaiwa kwamba wawili hao husagana.


TUKIO BICHI 
Madai
hayo ya muda mrefu huku wenyewe wakisisitiza si ya kweli, yameibuka
upya juzikati baada ya warembo hao kuonesha mahaba niue au nikongorowe
kisha ‘kudendeka’ hadharani na kusababisha mwandani wa Wema, Nasibu
Abdul ‘Diamond’ kukasirika na kuondoka eneo la tukio akiambatana na timu
yake ya Wasafi Classic Baby (WCB).


ILIKUWAJE?
Tukio hilo lililoshuhudiwa na wanahabari wetu lilijiri usiku wa kuamkia
Oktoba 28, mwaka huu ndani ya Mgahawa wa Rodizio, Masaki jijini Dar
ambapo Aunty alikuwa akisherehekea siku ya yake ya kuzaliwa ‘bethidei’.


WEMA ATOKEA DUBAI 
Shughuli
hiyo ilitawaliwa na matukio baada ya Wema kuwasili ukumbini hapo
akitokea nchini China kupitia Dubai alikokwenda hivi karibuni kwa
biashara binafsi ikidaiwa kwamba amerejea na mkwanja wa kutosha.


Wema
alitinga ukumbini hapo saa 7:15 usiku na kuwakuta wadau wakiendelea na
sherehe hiyo ambapo mara tu baada ya kufika alikumbatiana kimahaba na
 Aunty zoezi lililochukua dakika kadhaa wakiwa wamenasiana huku
wakifunika nyuso zao kwa zile nywele nyingi za Wema hivyo kilichoendelea
humo ndani hakikujulikana. Walipojifunua kwenye nywele ndipo ikabaini
kwamba kumbe walikuwa ‘wakidendeka’ bila kujali wingi wa kamera.


WASHUTUMIWA 
“Mungu
wangu, leo mambo hadharani. Mbona ni sheedah? Yaani wanadendeka
hadharani! Kwa vyovyote vile Wema na Aunty husagana,” alisikika mmoja wa
waalikwa.


Mmoja
wa waigizaji chipukizi alidakia: “Yaani utadhani wapenzi kabisa maana
kila mmoja anaonesha hisia za kumisiana. Hawaogopi kuambiwa wanasagana?
Haya bwana, yetu macho maana leo tutaona mengi. Vitendo kama hivi ni vya
kulaaniwa vikali na kuwakumbusha kwamba wao ni kioo cha jamii.”


DIAMOND AKASIRIKA, AONDOKA 
Kufuatia
 hali hiyo, Diamond alionekana kukasirika na kushindwa kuvumilia hivyo
aliamua kuwaacha wajinafasi kwa kuondoka ukumbini akiwa ameambatana na
timu yake. Waalikwa waliokuwa ndani ya ukumbi huo waliendelea kupigwa
butwaa na kitendo hicho hasa Diamond alipoamua kusepa huku nyuma Wema na
Aunty wakibaki huru na kuendelea kufanyiana mambo ya kimahaba mara
nyingine wakati wakilishana keki kwa staili ya njiwa.


AMANI LAMVAA AUNTY 
Baada
ya kuona hali hiyo, paparazi wa Amani aliyekuwa ukumbini hapo alimvaa
Aunty na kumuuliza kwa nini ameamua kuonesha hali hiyo mbele ya
kadamnasi ambapo alijibu hakuna mambo ya usagaji. Alisema hali hiyo
ilitokea tu maana yeye na Wema ni marafiki ambao wameshapitiliza hivyo
wamejikuta wakiwa kwenye hali hiyo bila wao kuona kama ni tatizo. “Kwani
nani asiyejua kama mimi na Wema ni marafiki, suala la kukisiana ni
jambo la kawaida kwetu.

GPL

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.