LEO NI ZAMU YA KUWAJUA MASTAA WA BONGO WANAOONGOZA KUTUKANWA MTANDAONI

Admin Updates10 years ago5 Views



Kwa upande wa wale ambao wanashika nafasi za juu kwa kutukanwa, wapo wengi lakini leo tutawazungumzia wahanga watatu.

Kajala Masanja:

Tangu aingie kwenye bifu na Wema Sepetu, kuna kundi ambalo linajiita
Team Wema limekuwa likimshambulia kwa kumtukana na kumshutumu kwa mambo
ambayo mengine hayana ukweli.

Hata hivyo, Kajala anaonekana kuwa mstaarabu kidogo kwani licha ya
kutukanwa mtandaoni, yeye amekuwa mkimya akijua kujibizana na watu hao
ambao wala hawana majina ni sawa na kuzidi kujichafulia.

Elizabeth Michael ‘Lulu’:
Huyu naye ni mhanga wa matusi mtandaoni. Kuna kundi la watu ambao
linaonekana kuwa na chuki dhidi yake, huenda kutokana na mafanikio
aliyonayo akiwa kwenye umri mdogo.

Lakini sasa, licha ya matusi anayoyaoga mtandaoni, amekuwa mvumilivu wa
kuyaacha yapite. Watu wake wa karibu wanaeleza kuwa, licha ya kutukana
sana mwenyewe wala hajui kwamba anatukanwa kwani si mtu wa kufuatilia
nani kasema nini kibaya juu yake

Wema Sepetu:

Kama ilivyo kwa Kajala, huyu naye anashambuliwa sana na Team Kajala.
Hawa ni watu ambao wamejitenga kuhakikisha wanamkosesha amani staa huyu.

Amekuwa akitukanwa kwa mengi lakini kwa kuwa anajua ustaa ni kama jalala, huwa hajali na anachukulia poa.

 Ni mara chache sana amekuwa akinyanyua mdomo wake kuwajibu wale ambao wamekuwa wakimsema vibaya sambamba na kumtukana.

Kwa uchache hao ndiyo mastaa ambao hivi karibuni wametia fora kwa

 kutukana na kutukanwa mtandaoni.

Tahadhari

Mastaa ambao ni wepesi kutukana mtandaoni  wajue kwamba endapo Rais wa
Jamhuri ya Muungano, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete atasaini ile sheria ya
makosa ya mtandaoni ya mwaka 2015, watajikuta wanaenda jela hivi hivi.

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.