Hamida Hassan na Imelda Mtema Katika
ulimwengu wa sanaa ya maigizo nchini, yupo mwanadada ambaye havumi sana
lakini yumo. Wengi wanamfahamu kwa jina la Muna lakini jina lake halisi
ni Rose Alfonce.Mwanadada huyo, mama wa mtoto mmoja, Patrick mwenye
miaka minne, ni ‘pacha’ wa msanii wa filamu, Ruth Suka ‘Mainda’. Amekuwa
akifanya mambo mengi ya kisanii na kijamii lakini si mtu wa kuuza sana
nyago kwenye magazeti.
Wiki hii Ijumaa lilimuweka mtu kati,
likamtaka azungumzie baadhi ya mambo ambayo watu wangependa kuyajua
ikiwemo malezi yasiyofaa anayodaiwa kumpa mwanaye, uhusiano wake na
mwanamuziki Kalala Junior pamoja na ukaribu wake na wasanii wenzake
Elizebeth Michael ‘Lulu’ na Mainda.
Mjue kwanza kidogo
“Kwenye
hili la uigizaji nilianza mwaka 2004 nikiwa ndani ya Kundi la Shirikisho
nilipoigiza kwenye tamthiliya zilizokuwa zikirushwa kwenye Televisheni
ya ITV ambazo ni Hatia na Siri.
“Ukiacha tamthiliya hizo, nilipata umaarufu sana kwenye filamu za Born to Suffer, Sekeseke, Siri ya Penzi na nyingine kibao.
Ahamia Haki Elimu
“Baada
ya kucheza filamu nyingi, nikabahatika kuingia kwenye matangazo
mbalimbali na mara ya mwisho niliingia kwenye yale ya Haki Elimu ambapo
nilionekana kama mwanafunzi.
Zaidi ya usanii
“Mbali na masuala ya uigizaji, sasa hivi nafanya biashara mbalimbali.
Ana undugu na Mainda?
“Mainda
siyo ndugu yangu kama baadhi ya watu wanavyofikiri, ni mtu wangu wa
karibu sana ambaye kwenye maisha yangu ya kisanii amechangia kwa kiasi
kikubwa. Ndiyo maana tunaitana mapacha.
Amzungumzia Lulu
“Wengi
wanakumbuka nilivyomsaidia Lulu alipokuwa gerezani na hata baada ya
kutoka nilikaa naye pale kwangu kwa siku kadhaaa. Yule pia ni zaidi ya
rafiki yangu na tumekuwa tukisaidiana kwa mengi.
Ni kweli yeye na Kalala Junior ni wapenzi?
“Naomba
hili nisilizungumzie kwa leo kwani nahisi ni mapema sana. Watu wanaona
tuna ukaribu sana na kila mmoja anahisi kivyake lakini niseme tu kwamba
muda ukifika nitaweka wazi kila kitu.
Kuhusu malezi ya mwanaye
“Nampenda
sana mwanangu Patrick, nipo tayari kufanya lolote zuri kwa ajili yake
na ndiyo maana watu wanasema namlea vibaya, wakumbuke kuwa mwanangu ni
staa hivyo kunyoa viduku, kuvaa kistaa siyo tatizo.
“Ameshacheza
filamu nyingi na kuonekana kwenye matangazo mengi na amesaini mkataba na
kampuni moja ya matangazo ambayo itamlipa dola 1,300 ambazo ni takriban
shilingi milioni mbili. “Nimemnunulia gari aina ya Passo na ameshaanza
kuiendesha. “Mwanangu napenda aje kuwa rubani,” anasema Muna.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33





