Tetesi hizo zimekuwepo kwa muda sasa japo wawili hao bado hawajaweza kuthibitisha muungano wao.
Mtangazaji namba moja kwa udaku nchini, Soudy Brown wa Clouds FM
alijaribu kumtafuta Jokate kutaka kutegua kitendawili hicho lakini kama
ilivyotarajiwa, Jokate aliishia kuangua kicheko tu na kutotoa jibu.
Wafuatiliaji wa mambo wameenda mbali zaidi na kudai kuwa wawili hao
wamekuwa wakionekana pamoja kwenye sehemu kadhaa ikiwemo nyumbani kwa
Alikiba.
Wengine wamefuatilia baadhi ya picha zao mitandao ya kijamii na kugundua kuwa Jokate amewahi kuivaa kofia ya mkeka ya Alikiba!
Bongo5 binafsi haijaweza kuthibitisha uwepo wa uhusiano huo.