
Baadhi ya viongozi wapya wa jeshi-usu la Uhifadhi wakila kiapo cha utii katika hafla ya kutunuku vyeo vipya kwa watendaji wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania. Hafla hiyo imefanyika katika Kituo cha Mafunzo ya jeshi-usu, Mlele mkoani Katavi.
Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA Dk. Allan Kijazi akishuhudia uvishwaji wa cheo kwa Naibu Kamishna wa Uhifadhi na Maendeleo wa TANAPA Wiliam Mwakilema uliofanywa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA Jenerali Mstaafu George Waitara
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara akimvisha cheo cha Kamishna Mwandamizi Kanda ya Kusini Dk Christopher Timbuka
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara akimvisha cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Mawasialino TANAPA Pascal Shelutete katika hafla ya uvishaji vyeo kwa Maafisa wa TANAPA.
Kamishna Msaidizi Huduma za Shirika Kanda ya Kusini Rukia Mkakile akiwa kwenye ukakamavu huku akipiga saluti kama heshima baada ya kuvishwa cheo hicho na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA Jenerali Mstaafu George Waitara ambaye hayupo pichani
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA Generali Mstaafu George Marwa Waitara akikagua gwaride la wahitimu wa mafunzo ya jeshi usu.
Wahitimu wa mafunzo ya jeshi-usu wakipita kwa mwendo wa haraka katika gwaride la utoaji wa vyeti kwa wafanyakazi wa TANAPA, Gwaride hilo lilikaguliwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA Jenerali Mstaafu ,George Waitara .
Baadhi ya watendaji wapya wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA Jenerali Mstaafu Geogre Marwa Waitara katika hafla ya kutunuku vyeo vipya kwa watendaji wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA
Picha ya pamoja ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA na Makamishna Wandamizi mara baada ya kuvikwa vyeo hivyo wakati wa halfa hiyo iliyofanyika katika kituo cha mafunzo ya jeshi-usu Mlele mkoani Katavi.from MICHUZI BLOG http://bit.ly/30ilIns
via






