Je wajua Tafsiri 17 Kuhusu Kuota Ndoto Upo Shuleni Unasoma Au Upo Shuleni Unafanya Mtihani Wakati Ulishamaliza Shule Miaka Mingi Iliyopita?SOMA HAPA
Awali ya yote ujumbe katika ndoto yoyote ile huwa unapatikana MWISHONI mwa ndoto wakati ndoto inaisha na sio MWANZONI mwa ndoto,
Hii ni ndoto ambayo imekuwa maarufu sana katika siku za hivi karibuni. Siku hizi karibu kila mtu mzima anaota ndoto hii. Sio mara moja wala sio mara mbili ni mara nyingi nyingi.
Wapo wanao ota ndoto hii walau mara moja au mbili kila mwezi, wengine huota mara moja kila wiki na wengine huota karibu kila siku. Wakati mwingine mtu anaweza kuota ndoto hii Zaidi ya mara moja ndani ya usiku mmoja na hali hiyo inaweza kujirudia mfululizo, yani mtu amelala tuseme saa nne usiku , saa sita usiku anaota ndoto hiyo, anastuka. Akilala tena anaiota ndoto hiyo hiyo.
Tuanze na ndoto ya kuota UPO SHULENI UNASOMA WAKATI WEWE ULISHAMALIZAGA SHULE MIAKA MINGI SANA IMEPITA.
Ulimaliza darasa la saba mwaka 1994 na kuendelea na masomo ya juu. Sasa hivi umeshakuwa mtu mzima mwenye watoto na pengine wajukuu kabisa. Lakini unalala usiku unaota ndoto umerudi shuleni katika darasa hilo hilo la saba au hata chini ya hapo. Upo katika mazingira ya shule ulio kuwa unaisoma. Katika ndoto yako hiyo mazingira ya shule yako huwa ni yale yale yaliyo kuwepo kipindi unasoma hata kama katika ulimwengu wa nyama yameshabadilishwa. Mfano kulikuwaga na miti mikubwa labda sasa hivi imeshakatwa. Kulikuwa na sehemu ya wazi na sasa hivi imejengwa madarasa mengine. Wewe katika ndoto yako utakuwa katika mazingira yale yale yaliyo kuwepo mwaka huo wa 94 wakati bado unasoma katika shule hiyo.
JE NDOTO HII INA MAANA GANI ?
Dhana iliyo jengeka miongoni mwa watu wengi katika jamii ni kwamba ukiota ndoto hii basi maana yake ni kwamba kuna watu wanakurudisha nyuma kwa kutumia uchawi. Yani kwa lugha nyepesi kuna watu wanakufunga kichawi ili usipate maendeleo. Uendelee kubakia hapo hapo ulipo na uzidi kurudi nyuma kimaisha.
JE TAFSIRI HII NI SAHIHI ?
Jibu langu ni NDIO na HAPANA. Ndio kwa maana ya kwamba ukiota ndoto umerudi shuleni inaweza kuwa ina maanisha kwamba kuna watu wanakufunga kwa lengo la kukurudisha nyuma kimaendeleo lakini HAPANA kwa maana ya kwamba si kila unapo ota ndoto umerudi shuleni basi tafsiri yake ni kwamba kuna watu wanakuroga kwa lengo la kukufunga ubaki hapo hapo ulipo na kukurudisha nyuma.
Ndoto hii ina tafsiri nyingi sana. Kuipa tafsiri moja tu kama watu wengi wanavyo amini ni kuto kuitendea haki ndoto hii na ulimwengu wa ndoto kwa ujumla wake.
Kama nilivyo dokeza hapo juu, ndoto hii ina tafsiri nyingi sana. Baadhi ya tafsiri muhimu kuhusu ndoto hii ni kama ifuatavyo ;
Ulevi, uzinzi na uasherati pamoja na anasa za dunia ni miongoni mwa tabia na mienendo ambayo inarudisha nyuma maendeleo ya watu wengi sana . kama wewe unajihusisha na tabia hizo hapo juu halafu ukawa unaota ndoto umerudi utotoni basi ni ishara kwamba tabia na mwenendo wako vinakurudisha nyuma kimaendeleo. Tabia na mwenendo wako ndio mchawi wako namba moja.
2.TAFSIRI NAMBA MBILI : NI ISHARA YA KUKUONDOA HOFU JUU YA JAMBO ULILO LIFANYA AU LILILO KUTOKEA AMBALO LIMEKUFANYA UWE NA HOFU KUBWA SANA KATIKA MAISHA YAKO.
Mfano umekutana kimwili na mtu bila kutumia kinga halafu baadae ukasikia mtu huyo aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na muathirika, jambo hili linaweza kukupa hofu kubwa sana kwenye nafsi kiasi cha kukata tamaa ya kuishi duniani kwa kuamini na wewe umeathirika na mwisho wa siku unaweza kujiingiza katika tabia za hatari zaidi kama kuendelea kufanya ngono nzembe na watu mbalimbali huku ukiamini kwamba wewe ndio unawasambazia . Matokeo yake basi katika mchakato huo wa kuwaambukiza na kuwasambazia watu virusi, wewe ndio unaweza ukajikuta unaambukizwa. Malaika walinzi wako kwa sababu wana uwezo wa kusoma nyota yako na kujua mambo yatakayo kutokea mbeleni, wataanza kukupa ujumbe wa kukutoa hofu kwa njia ya ndoto. Ukiwa katika hali kama hii halafu ukaanza kuota ndoto umerudi utotoni basi maana yake ni kwamba jambo unalo lihofia halipo. Yani kwa suala la usalama wa damu yako, damu yako ni salama kama ilivyo kuwa miaka mingi iliyo pita wakati upo utotoni. Hapa malaika walinzi wako wanakuwa wameisoma nafsi yako ambayo inatamani siku zirudi nyuma. Hivyo wanakujibu kwa njia ya ndoto kwa kukurudisha nyuma kwa njia ya ndoto.
Hapa malaika walinzi wako wakiona huelewi kwa njia ya ndoto, wataanza kukupa ishara nyingine za kawaida. Kwa mfano uta kuwa unatembea mjini mara unakutana na rafiki yako ambae mlisoma wote shule ya msingi na kwa mara ya mwisho mlionana miaka kumi iliyopita ( kipindi ambacho hukuwa na hofu kama uliyo nayo leo hii ). Unatoka hapo unaenda kupanda kwenye gari unasikia zinapigwa nyimbo za miaka 25 iliyo pita wakati upo darasa la tatu nakadhalila . ( Ukiona hivyo basi jua unapewa taarifa kwamba jambo unalo lihofia halipo wala halijakutokea kwa hiyo usiwe na hofu yoyote kuhusu jambo hilo )
4.TAFSIRI NAMBA NNE : UNAPEWA ONYO USIRUDIANE NA MTU ULIE KUWA UMEACHANA NAE.
Ulikuwa na mke, mume , mchumba au mpenzi halafu mkatengana. Baada ya muda Fulani, mke, mume, mchumba au mpenzi huyo akakuomba mrudiane. Ukiwa katika mchakato wa kutaka kurudiana nae unaanza kuota ndoto umerudi shuleni au utotoni. Tafsiri ya ndoto hiyo ni kwamba endapo utarudiana na mke, mume, mchumba au mpenzi huyo basi jambo hilo litakurudisha nyuma sana kimaisha. Malaika walinzi wako kwa sababu wana uwezo wa kuona mambo yatakayo kutokea mbeleni wanakupa tahadhari hiyo kwa njia ya ndoto.
Sababu zinaweza kuwa mke, mume, mpenzi, au mchumba huyo ana laana na vifungo vya kimasikini vya ukoo, familia au kijiji. Ukifunga nae ndoa au ukiwa nae katika mahusiano ya kimapenzi maana yake na wewe unakuwa umeunganishwa kwenye laana na vifungo vyake.
Vile vile sababu zinaweza kuwa tabia za mwanaume huyo zitakurudisha nyuma kimaendeleo. Kwa mfano inawezekana wewe unafanya kazi au shughuli inayo kuingizia kipato ambacho unakitumia kukidhi haja zako na kuwasaidia familia yako halafu huyo mwanaume yeye hataki kuoa mwanamke ambae anafanya kazi. Yeye akikuoa atataka uwe mama wa nyumbani. Atakuachisha kazi na hatotaka ufanye biashara yoyote na anaweza kutumia fursa hiyo kukunyanyasa pia na mwisho wa siku utaishia kuachana nae huku ukiwa umepoteza muda wako mwingi sana ukiwa nae. NDIO MAANA UNAPEWA ONYO USIRUDIANE NAE.
5. TAFSIRI NAMBA TANO : NI ISHARA KWAMBA MARADHI YA KICHAWI YALIYO KUWA YANAKUSUMBUA YAMEPONA.
Kama ulikuwa umetupiwa maradhi ya kichawi na yakakutesa kwa muda mrefu halafu baadae ukapata tiba ya kuondosha maradhi hayo basi kuna uwezekano mkubwa sana kuota ndoto umerudi utotoni.
Hii maana yake ni kwamba, maradhi yako yote yameondoshwa na sasa umekuwa mpya. Umerudi kwenye upya., Kwa hiyo kama upo kwenye kundi hili halafu ukaota ndoto umerudi utotoni basi maana yake ni kwamba wewe umekuwa mpya.
6.TAFSIRI NAMBA SITA : NI ISHARA KUWA NYOTA YAKO ILIYO KUWA IMEIBIWA AU KUCHAFULIWA SASA IMERUDISHWA.
Kama nyota yako ilikuwa imechukuliwa halafu ikarudishwa basi kuna uwezekano mkubwa wa wewe kuota ndoto umerudi utotoni.
Hii maana yake umekuwa mpya. Nyota yako imekuwa swafi kama ulivyo kuwa mtoto mdogo. Ukiachilia mbali kurogwa, nyota ya mtu huwa ina haribiwa na zinaa. Unapo fanya zinaa una haribu nyota yako kwa sababu una unganisha nafsi( nyota ) yako na nafsi ( nyota ) ya mtu unae fanya nae zinaa. Katika ulimwengu wa kiroho, watoto wadogo ni alama ya nyota inayo ng’aa ama nyota iliyo kamilika, nyota safi.
Sasa kama nyota yako ilikuwa imechafuliwa, imekufa, imeshushwa, imefungwa au ime imechukuliwa ( imeibwa ) halafu ukarejesha nyota yako. Ukiota ndoto umerudi utotoni maana yake ni kwamba nyota yako iliyo kuwa imeibwa sasa imerudi. Na kama wewe ni mwanamke basi tunasema umerudi kwenye ubikira. Umekuwa swafi.
7. NI ISHARA KWAMBA PESA ULIYO IPATA HIVI KARIBUNI ITAISHA YOTE BILA WEWE KUFANYA KITU CHOCHOTE CHA MAANA :