Mwanza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Mohamed Mchengerwa ametangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika shule mbalimbali za Serikali nchini mwaka wa masomo 2024.
Angalia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza HAPA
Majina hayo yanajumuisha ya wanafunzi waliochaguliwa kwenda kusoma shule za sekondari za bweni, vipaji maalum na kutwa za Serikali.
Mchengerwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa, wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga shule za kutwa wanaripoti shuleni ifikapo Januari 8, 2024 huku waliochaguliwa shule za bweni wakitakiwa kuripoti ifikapo Januari 6, 2024.
Waziri huyo amesema hayo leo Jumapili, Desemba 17, 2023, jijini Mwanza alipozungumza na waandishi wa habari.