Malkia wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ siku ya jana anadaiwa ametolewa mahari na mpenzi wake wa muda mrefu Majay ikiwa ni maandalizi ya ndoa yao mwisho wa mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa Wa Dar Es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda katika ukurasa wake wa instagram atoa pongezi kwa kuandika, “Mafanikio yenu yamebeba watu wengi, na kila hatua inaonyesha hamtanii basi Mungu wangu aendelee kuwaonyesha njia ili mfikapo mkawe msaada na kwawengine.”
Mastaa kibao walikuwepo kuhudhuria sherehe hiyo ya kutolewa mahali kwa Lulu jambo ambalo ni hatua mpya kuelekea ndoa yao inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.