TUJIUNGE LEADERS
Matukio hayo ya kusisimua yaliwatia hofu kubwa mashabiki na wadau wa
muziki Bongo muda mfupi kabla ya nyota hao kukaribishwa stejini kwenye
Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar, mwishoni mwa wiki
iliyopita.
HIRIZI ZAKUTWA UWANJANI
Kwa mujibu wa wanahabari wetu, katika Viwanja vya Leaders, Kinondoni,
kulikutwa hirizi zilizozagaa, zilizodaiwa kudondoshwa na vijana
waliokamatwa wakiwa wamevalia sare zenye majina ya mastaa hao wawili.
Katika hali ya kushangaza, mmoja wa mashabiki waliohudhuria onyesho hilo
ambaye aliziona hirizi hizo, aliwashangaza mashabiki wenzake alipodai
kuwa anaiona mojawapo ikitweta mithili ya inayopumua!
“Oneni wadau, hii hirizi si inapumua, iangalieni vizuri,” alisikika
shabiki huyo na kuwaacha watu wakiwa wamepigwa na butwaa kuona vitendo
hivyo vya kishirikina katika eneo la burudani.
Pamoja na Diamond kula mwereka hadi chini, hali ilizidi kuwa mbaya kwake
baada ya muziki kuanza kusikika vibaya huku ukiwa unakatakata, kitendo
kilichoamsha hisia kuwa kulikuwa na ushirikina unaoendelea ili kumshusha
kisanii kwa kuonekana amefanya vibaya katika shoo hiyo
CHUPA ZARUSHWA
Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya huku chupa za maji zikirushwa
jukwaani hapo na baadhi zikimpiga na nyingine akizikwepa wakati
akiendelea kupiga shoo, Diamond aliamua kutumia akili ili kuzima kelele
hizo kwa kuanza kumwaga noti.
Ishu hiyo iliwafanya mashabiki na Timu Kiba kuachana na zoezi hilo na
kuanza kusukumana kugombea noti hizo za elfu mbilimbili ambapo alimwaga
kwa awamu tatu.
SADAKA?
Wakati akizidi kuwatupia noti mashabiki, Diamond alisikika akisema kuwa
pesa hizo ni maalum kwa mashabiki kwani ni sadaka kwao kutokana na
sapoti kubwa wanayompa ingawa hataweza kumpa kila mmoja.
DIAMOND KAMA MICHAEL JACKSON
Hata hivyo, baadhi ya mashabiki waliokuwa wakisukumana na kuokota noti hizo walisikika wakisema:
“Huu mchezo alikuwa akiufanya Michael Jackson (Mwanamuziki marehemu wa Marekani) tena alikuwa akitumia ushirikina na Freemasons.
“Michael alikuwa anadaiwa kumwaga fedha hizo zilizokuwa na nguvu ili
kuwafanya wale waliokuwa wakimzomea kukaa kimya,” alisikika shabiki
mmoja akisema.
MSHANGAO
Katika hali ya kushangaza zaidi, Diamond alivua tisheti na vesti ya
ndani na kujifuta jasho kisha kuwarushia mashabiki huku akijua wazi kuwa
amefutia jasho lililokuwa likimiminika mwilini mwake kama maji.
KIBA HAKUTAKIWA KUZUNGUMZA?
Wakati matukio ya kushangaza aliyokuwa akiyafanya Diamond na yale ya
kurushiwa chupa za maji machafu na yenye mikojo yakiendelea, ilidaiwa
kuwa Kiba alipoingia kwenye chumba cha wasanii hakutaka kuzungumza na
mtu yeyote huku ikidaiwa kuwa hiyo ni ishara kubwa kuwa hakutakiwa
kuzungumza na mtu kwani angeweza kupoteza nguvu za kufanya shoo.
POLISI MZIGONI
Wakati mashabiki wakizidi kuwa na wasiwasi juu ya wasanii hao, jeshi la
polisi lililokuwa na zana zote za kukamatia wahalifu, walianza doria ya
kukamata vijana ambao wanadaiwa kuwa ni Timu Kiba waliokuwa wakibishana
na kutupa chupa zenye mikojo na maji huku wakipokea kipigo kama cha
mbwa mwizi.
KIBA ARUKA UKUTA
Awali kabla ya shoo hizo kuanza matukio ya kishirikina yalijidhihirisha
zaidi baada ya Ali Kiba kuingia uwanjani hapo kwa njia ya kuruka ukuta
na hata alipozama kwenye chumba maalum walichokuwa wametengewa wasanii
hakuweza kushikana mikono na wenzake.Wasanii ambao Ali Kiba aliwachunia
ni AY, MwanaFA, Shaa, Shilole, Vanessa Mdee na Jux, ambao wote aliwakuta
ndani ya chumba hicho.
Imeandaliwa na Gladness Mallya, Musa Mateja, Chande Abdallah, Mayasa Mariwata, Shani Ramadhani, Denis Mtima na Laurent Samatta