Gamondi Atamba: Ninawasoma Vital’O, nataka tuwapiga nje ndani

Admin Updates11 months ago6 Views

 

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miguel Angel Gamondi amesema kuwa jambo analotaka ni timu yake kutinga hatua ya makundi kwanza kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika kabla ya mambo mengine kuendelea, hivyo anao wajibu wa kufanya vizuri kwenye hatua za awali ili afikie makundi.

Gamondi amesema kuwa anajiandaa kutoa kipigo kizito kwa Vital’O ya Burundi ambao wamepangwa nao kwenye hatua ya kwanza ya mtoano kabla ya kwenda kukutana na mshindi kati ya SC Villa ya Uganda dhidi ya Commercial Bank ya Ethiopia.

“Hakuna kingine zaidi ya kushinda na kwenda hatua inayofuata. Kila mechi tunataka kushinda, hii ni knockout stage tutacheza nyumbani na ugenini lazima tushinde mechi zote ili twende mbele, malengo yetu ya kwanza ni kwenda hatua ya makundi.

“Hii ndiyo sababu iliyonifanya nikaja hapa msimu uliopita na ndiyo sababu iliyonibakisha msimu huu kwa sababu ninataka kupambana kwenye mashindano makubwa Afrika na kuwaonesha kuwa Tanzania inaweza kufanya vizuri kwenye michuano mikubwa Afrika hususani CAFCL.

“Sijawahi kucheza na timu yoyote ya Burundi lakini nilishawahi kufika Burundi kutazama mechi moja ya timu ya Taifa ya Burkina Faso. Kwa sasa tutaanza kuifanyia uchunguzi na kuwasoma kimbinu Vital’O na nchi ya Burundi kwa ujumla.

“Kwa vile sio mbali ninaamini Wananchi watakuwa wengi huko Burundi kama walivyofanya msimu uliopita walipotufuata Rwanda wakati tukicheza na El Merrikh,” amesema Gamondi.

Mechi za mkondo wa kwanza wa hatua ya awali zitapigwa kati ya Agosti 16 – 18 huku marudiano yakitarajiwa kupigwa kati ya Agosti 22 – 25, 2024.

Mechi mkondo wa kwanza wa raundi ya kwanza zitapigwa kati ya Septemba 13-15, 2024 huku marudiano yakitarajiwa kupigwa kati ya Septemba 20-22, 2024

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.