Fisi Aliyeua Watu Wawili na Kujeruhi Watano Auawa

Admin Updates2 years ago5 Views

 

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imefanikiwa kumuua fisi aliyeua watu wawili na kujeruhi watano katika wilaya ya Lindi Vijijini mkoani Lindi.
Kamanda wa Uhifadhi wa Kanda ya Kusini Mashariki, Abraham Jullu amesema mnamo tarehe 11 Mei, 2023 majira ya saa kumi na mbili asubuhi, ofisi yake ilipokea simu kutoka kwa Mtendaji wa Kata ya Milola, akitoa taarifa kuwa fisi amejeruhi watu watatu katika Kijiji cha Rutamba, watu wawili Kijiji cha Ng’apa na kusababisha vifo vya watu wawili.
Amewataja waliojeruhiwa na fisi huyo kuwa ni Suleman Mtambo, Hadija Said, Alpha Ibrahimu, Maria Sabuni na mwingine aliyetambulika Kwa jina moja la Steven ambao wote walipelekwa Hospitali ya Sokoine mkoani Lindi, huku waliofariki walitambulika kwa majina ya Abilahi Pokosoi, na Saidi Makolela.
Kamanda Jullu amesema baada ya kupokea taarifa hiyo, mara moja alituma kikosi cha askari wapatao watano kwa ajili ya kumsaka fisi huyo ambapo baada ya msako…majira ya mchana askari hao walifanikiwa kumuona na kumuua.
Aidha, Kamanda Jullu amesema taratibu za kuwasaka fisi wengine katika maeneo mbalimbali ikiwemo Milola na vijiji vya Wilaya ya Ruangwa zinaendelea na kuona namna bora ya kuwahamisha na kuwapeleka maeneo ya hifadhi.
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.