Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamiii
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dkt.Hassan Abass amesema serikali imekuwa matokeo mazuri katika mapato kutokana mabadiliko ya mifumo mipya pamoja na mabadiliko ya Sheria katika sekta ya madini.
Abass ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi habari ikiwa ni utaratibu wa kila mwezi kutoa taarifa za serikali.
Amesema serikali imepata kodi inayotokana na madini sh.bilioni 300 kwa mwaka wa Fedha 2018/2019.Amesema mapato hayo ya kodi yanatokana na matokeo ya utungaji wa sheria za madini na kufanya Tanzania kunufaika na sekta hiyo.
Amesema pamoja na sheria hiyo pamoja na serikali kuagiza kuanzisha kwa masoko ya madini kilo zimeongezeka ikilinganishwa na miaka nyuma.
Abass amesema Geita kabla ya soko walikuwa wanapata kilogram za Madini 259 baada ya soko kuanzisha ni kilogram 312 na maeneo mengine yameendelea kufanya vizuri katika masoko ya madini.
Amesema kabla ya ukuta wa merelani kujengwa zilikuwa zinapatikana kilogram 164 hadi kufikia kilo 781 baada ya ukuta kujengwa.Dkt. Abass amesema Tanzania inakwenda katika mageuzi ya kiuchumi katika sekta ya Madini katika Afrika na Dunia kwa ujumla.
Amesema wale wanaopinga kwa kutumia mitandao katika juhudi za serikali wanaumbuliwa na matokeo yanayotokea.
Amesema baada ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli kupokea mtambo wa TTMS kwa serikali imepata mapato zaidi ya sh.bilion 97 katika miamala ya machi watanzania walitumiana miamala ya Fedha zaidi ya sh. Bilioni Moja.
Hata hivyo katika mfumo wa malipo ya huduma mbalimbali za serikali zaidi taasisi 400 zimejiunga.
Amesema shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) tangu kujiunga imeokoa sh.bilioni 38 huku wakala wa Vipimo wakifikia bilioni mbili kutoka bilioni Moja na Aridhi kutoka sh.milioni 70 hadi sh.milioni 100.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dkt.Hassan Abass akizungumza na waandishi habari kuhusiana na masala mbalimbali yaliyotokea Serikalini jijini Dar es Salaam.
from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2HKN91P
via