

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.Faustine Ndugulile akikagua nyaraka mbalilmbali wakati alipotembelea kukagua maabara katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akikagua nyaraka mbalilmbali wakati alipotembelea kukagua stoo ya dawa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia mfuko unatumikia kuweka unga lishe unaotengenezwa na Kiwanda cha Ruaha Milling mkoani Iringa wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akimpima mtoto uzito katika siku ya lishe katika eneo la Tanangozi mkoani Iringa wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akishiriki kupika uji lishe kwa ajili ya watoto katika katika siku ya lishe katika eneo la Tanangozi mkoani Iringa wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akisikiliza taarifa ya mkoa kutoka kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Atupele Mwandiga wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani Iringa kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii mkoani humo.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akisalimiana na kuzungumza na mzee aliyekutana naye akipatiwa huduma katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii.
…………….
Na Mwandishi Wetu Iringa
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amemuagiza Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Atupele Mwandiga kuhakikisha anapata taarifa ya utoaji wa dawa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa.
Agizo hilo limekuja mara baada ya ziara ya yake mkoani humo alipotembelea hospitali hiyo kujionea utoaji wa huduma za afya kwa wananchi na kushuhudia mmoja wa mama aliyejifungua Hospitalini hapo kupewa dawa mara moja badala ya mara tatu kama iilivyoandikwa na Daktari.
Dkt. Ndugulile amesema kuwa amekasirishwa na utendaji kazi wa manesi katika wodi ya Mama na Mtoto kwa kutozingatia utoaji huduma hasa kuhakikisha wazazi na watoto wanapewa dawa kwa wakati zinazotakiwa na kwa idadi sahihi.
Ameongeza kuwa lengo la mgonjwa kupewa huduma ni kuhakikisha anapona na sio kufanya aendelee kupata tabu na shida hivyo Serikali ya Awamu ya Tano imewekeza fedha nyingi katika kuhakikisha Sekta ya Afya inaboreshwa nchini.
“Haiwezekani mgonjwa kanunua dawa zake kwa fedha zake lakini bado hata hamzingatii kumpatia dawa mnategemea ataponaje” alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha Dkt. Ndugulile ameutaka uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa kuhakikisha wanaratibu utoaji wa huduma hospitalini hapo ili kuepukana na malalamiko ya wagonjwa na kupoteza imani ya wananchi kwa Hospitali hiyo.
“Tukiendelea hivi tutaondoa imani kwa wananchi wetu katika utoaji wa huduma za afya sisi tunatakiwa kutoa huduma kwa wananchi na sio kuwapa kero wananchi” alisema Dkt. Ndugulile.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Atupele Mwandiga amemuahikikishia Naibu Waziri Dkt. Ndugulile kusimamia utoaji huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa na kusimamia vilivyo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma inayostahili.
Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya tano imetoa kiasi cha Billioni 7 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Wilaya na maboresho katika Zahanati na vituo vya Afya mkoani humo katika kuhakikisha inaboresha Sekta ya Afya hivyo watasimamia Sekta hiyo kikamilifu.
“Mhe. Naibu Waziri tutahakikisha hatutopoteza imani ya wananchi katika utoaji huduma za afya na tutatendea haki rasimali fedha tulizopewa na Serikali katika kuboresha Sekta ya Afya Mkoani kwetu” alisema Dkt. Atupele
Wakati huo huo Dkt. Ndugulile ametembelea na kujionea utendaji kazi utoaji wa huduma kwa wananchi katika Ofisi ya Bima ya Afya (NHIF), Kampeni ya masuala ya Lishe, Kiwanda cha Ruaha Milling na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kilolo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile yuko katika ziara ya siku mbili mkoani Iringa kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii mkoani humo.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2N51sAG
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







