Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, amewaongoza watendaji wa Wizara hiyo kumpokea Naibu Katibu Mpya, Kamishna Benedict Wakulyamba, ambaye awali mapema leo aliapishwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuanza kazi hiyo.
Kamishna Wakulyamba anachukua nafasi ya Bw. Anderson Mutatembwa ambaye amehamia Ofisi ya Waziri Mkuu.