wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amefanya tukio la
kihistoria kiasi cha kumliza mama yake mzazi, Sanura Kassim ambaye
alimwaga machozi kama mtoto mbele za watu.
Tukio la mama Diamond
kumwaga machozi lilishuhudiwa na kamera za Amani, juzi Jumatatu, mishale
ya saa mbili usiku nyumbani kwake, Sinza jijini Dar es Salaam ambako
kulikuwa na ‘bethidei’ ya mama huyo.
Waalikwa na mama huyo, wote
walijua kuwa shughuli ilikuwa ni futari lakini kumbe nyuma ya pazia
kulikuwa na tukio la kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mama huyo ambayo
inadaiwa alikuwa hakumbuki.
Mmoja wa rafiki wa karibu na familia
hiyo, kwa sharti la kutotajwa jina lake , alisema kuwa hadi jioni, mama
Diamond hakuwa akifahamu kuwa aliandaliwa sherehe ya siku yake ya
kuzaliwa.
“Mipango yote
ilifanywa kwa siri mama Diamond hakujua kilichoendelea. Diamond akiwa
Marekani alitoa maelekezo mama yake afanyiwe shughuli hiyo hata kama
hayupo kwa sababu siku ya kuzaliwa haijirudii,” alisema rafiki huyo.
KILICHOMLIZA
Muda
mfupi baada ya shughuli ya kufuturu kukamilika, mama Diamond alishangaa
kusikia kwamba kulikuwa na jambo jingine la ziada katika siku hiyo.
Alitolewa nje huku akiimbiwa ‘happy birthday’ ndipo alipogundua
kilichokuwa kikiendelea.
Mara baada ya shampeni isiyo na kilevi
kufunguliwa na waalikwa kupewa, meneja wa Diamond, Babu Tale na wapambe
wengine walimuongoza mama huyo hadi kwenye gari aina ya Toyota Lexus
Harrier na kuelezwa kuwa ni mali yake kuanzia muda huo tamko
lililomshtua na kuanza kulia akiwa haamini alichosikia!
“Siamini
macho yangu, siamini… asante sana mwanangu (Diamond), nakuombea kila
kukicha mwanangu uwe na afya njema, unilee kwa upendo, asante Mungu,” alisikika mama Diamond akitamka kwa sauti iliyoambatana na kilio cha nguvu.
Muda huohuo akafunguliwa mlango na kuingia ndani ya gari hilo lililopambwa ndani kwa vitu kibao vya thamani.
WEMA, AUNT WAMBEMBELEZA
Machozi
ya mama Diamond hayakukoma hata baada ya kushuka ndani ya gari,
alionekana kuchanganyikiwa kama siyo kutoamini sapraizi ya mwanaye,
ndipo Miss Tanzania 2006, aliye pia mchumba wa mwanaye, Wema Sepetu na
staa wa filamu za Bongo, Aunt Ezekiel walipovaa jukumu la kumtuliza.
Mastaa
hao ambao ni mtu na shogaye, walimchukua mwanamke huyo na kwenda naye
pembeni ambako walimsihi atulie na akubaliane na alichokiona kwani ndiyo
ukweli wenyewe.
Juhudi zao zilizaa matunda, kwani muda mfupi
baadaye mama Diamond alifuta machozi na kurudi katika hali yake ya
kawaida ingawa alishindwa kuficha furaha yake.
DIAMOND, WEMA NDOA LAZIMA!
Katika
kuonesha kuwa sasa amekubali kwa dhati Wema awe mkwewe, mama Diamond
aliapa lazima ahakikishe mwanaye anafunga ndoa na mlimbwende huyo.
“Hilo nataka mlijue kabisa. Nitafanya juu chini Diamond amuoe Wema maana ana roho nzuri sana. Niseme ukweli kuwa huyu msichana ndiye chaguo langu na wanaendana sana na mwanangu.
“Angalia
wakiwa pamoja, mwanangu anapata mafanikio makubwa sana, nadhani nyota
zao zinaendana hivyo sina pingamizi lolote. Ninachotaka ni kuhakikisha
wanaoana,” alisema mama Diamond.
THAMANI YA GARI
Akizungumzia
thamani ya gari hilo, Babu Tale alisema ni shilingi 34,000,000 (milioni
34) ikiwa ni pamoja na mazagazaga mengine baada ya gari hilo
kununuliwa.

Gazeti la Amani/ Gpl