mwongozaji na mwigizaji wa filamu Bongo, Adam Philip Kuambiana, daktari
mkubwa wa mastaa ameibuka na kudai marehemu alijiua mwenyewe.
gazetini kutokana na maadili ya taaluma yao kuficha siri ya mgonjwa,
siku moja kabla ya kifo (Ijumaa ya Mei 16, mwaka huu), marehemu
alimpigia simu na kumwambia amekunywa dawa za malaria aina ya Fansidar
lakini pia amekunywa pombe.
ILIVYOKUWA
juu ya nini cha kufanya na kama kuna madhara yoyote juu ya pombe hizo na
dawa alizokunywa.
“Aliniuliza kama kuna madhara yoyote ambayo
anaweza kuyapata kwa kuwa alikuwa amekunywa fansidar kwa ajili ya
malaria kisha akapata kiu ya bia na kuamua kunywa,” alisema daktari huyo.
AMSHAURI KWENDA HOSPITALI
licha ya msanii huyo kuwa na ‘masikhala’ mara kwa mara, lakini kwa kuwa
alimwambia jambo ambalo linahusu uhai wake, alimshauri kwenda hospitali
iliyo karibu ili akaonane na daktari kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa
kutoa sumu kwani kitaalam mtu anapokunywa pombe akiwa amemeza dawa za
aina hiyo vyote hugeuka kuwa sumu.
Alisema kutokana na jinsi alivyozidi kumsimulia hali
aliyonayo, aliamini kwamba marehemu alikuwa anamaanisha alichokuwa
akikisema hivyo ikabidi amsisitize kuwahi hospitali haraka.“Nilimwambia awahi hospitalini haraka kwani nilijua fansidar
ni kali na si dawa ya kufanyia mchezo. Lakini kesho yake nilipopata
taarifa za kifo chake niliumia sana japokuwa nilijua amejiua kwa
kuchangaya fansidar na bia maana mchanganyiko wa sumu yake mwilini ni
mkali sana,” alisema daktari huyo huku akisisitiza kusitiriwa kwa jina lake.
MAZINGIRA YA KIFO
ambaye naye hakutaka kutajwa jina gazetini, marehemu asingekufa ghafla
kama tatizo alilokuwa nalo lingekuwa la vidonda vya tumbo ambavyo
vilikuwa vikimsumbua kwa muda mrefu.
“Siku ile marehemu alikuwa na pesa, alikunywa
sana pombe kutoka asubuhi mpaka usiku mwingi, alikuwa anakula kila
anapojisikia sasa hatuelewi ni kitu gani kilitokea maana haiwezekani mtu
akutwe anaendesha na kutapika damu pasipo kuwa na sumu mwilini,” alisema mtu huyo.
DAKTARI AWAASA MASTAA
makini kwani mara kadhaa amepata kesi za namna hiyo ambapo wanakunywa
pombe vilabuni usiku huku wakiwa katika dozi ya ugonjwa fulani.
“Mimi nawaambia ndugu zangu, hasa mastaa waache
tabia ya kunywa pombe wakiwa katika dozi, starehe zipo tu. Ni vyema
wakawa wanauliza kwa wataalam wa afya pindi wanapokuwa wamemeza dawa za
aina yoyote, nguvu ya dawa inatofautiana kulingana na ugonjwa husika na
muda wa kukaa mwilini,” alisema daktari huyo.
DAKTARI MUHIMBILI ANENA
lilimtafuta daktari mwingine mtaalam wa magonjwa ya binadamu wa
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Naye kwa sharti la kutotaja jina
alieleza madhara ya mtu kunywa pombe akiwa kwenye dozi.
“Unapokunywa dawa hususan hiyo fansidar, inakaa
katika mwili kwa takriban siku saba hivyo mgonjwa anapokunywa pombe
ndani ya siku hizo, pombe inapochanganyika na dawa katika mzunguko wa
damu hugeuka kuwa sumu na mgonjwa ana uwezekano wa kupoteza maisha
endapo asipowahishwa hospitalini,” alisema daktari huyo na kuongeza:“Wengi huwa wanajisahau na
kunywa pombe kabla ya siku saba lakini wengine huwa wanakunywa pombe
makusudi pale tu wanapoanza kupata ahueni ya ugonjwa pasipo kutambua
nguvu ya dawa bado ipo mwilini mwake na madhara yake ndiyo hayo.”
JB AANGUKA GHAFLA, AZUA HOFU
Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar, nguli wa filamu nchini ambaye
alikatisha ziara yake ya kikazi nchini Uturuki kwa ajili ya kuja
kumzika Kuambiana, Jacob Steven ‘JB’, alipewa kipaza sauti ili
amzungumzie marehemu ambapo akiwa katikati ya kuongea alianguka ghafla.
kuelewa amepatwa na nini lakini haikuchukua muda mrefu akasaidiwa na
watu na kuendelea na shughuli nyingine.
MASTAA WAONGOZA KWA VILIO
‘Beautiful Onyinye’, Aunt Ezekiel, Blandina Chagula ‘Johari’, Miriam
Jolwa ‘Jini Kabula’ waliongoza kwa kulia viwanjani hapo hadi walipofika
makaburini, Kinondoni.
alijikuta akishindwa kuaga kwa kuhofia kuuona mwili wa marehemu na kudai
huwa akitazama maiti anamuota kwa zaidi ya mwezi mmoja.
filamu, alipatwa na mauti katika Gesti ya Silvarado, Sinza- Kwaremmy
jijini Dar. Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amina.

