Serikali ya China,imemuonya Rais Mteule wa Marekani Donald Trump,kutofanya jambo lolote kinyume na Sera ya nchi hiyo ya ”One China Policy” kuhusu Taiwan,ya kisiwa hicho kuwa ni sehemu ya China,na kwamba atavuna atakachopanda.
Onyo hilo limetolewa na msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo GENG SHUANG,kufuatia matamshi ya bwana Tramp,kuwa Marekani itaendelea kutambua Taiwan,kuwa sehemu ya China kwa masharti.
Msemaji huyo wa Wizara ya mambo ya nje ya China,amemtahadharisha bwana Trump,kulichukulia kwa tahadhari suala la China,kama vile glasi ama yai,la sivyo,atauharibu uhusiano baina ya pande mbili hizo kwakuwa China,haitakubali kuingiliwa mambo yake ya ndani na utaifa wake.
Awali Rais Mteule wa Marekani Donald Trump,amesema,Marekani,haioni ulazima wa kusimamia msimamo wake wa muda mrefu kuwa Taiwan,ni sehemu ya China na kuhoji msimamo huo wa miongo minne.
Matamshi hayo ya bwana Trump,aliyoyatoa katika mahojiano maalum na chombo kimoja cha habari nchini Marekani,ndiyo yaliyoibua hasira ya China,na yenyewe kutoa tahadhari kwake.
Matamshi ya Trump,yaliyolenga kujitetea,yamefuatia China,kupinga kidiplomasia,hatua ya bwana Trump,kuhusiana na uamuzi wake wa kupokea simu ya Rais wa Taiwan Desemba 2 mwaka huu.
Katika mahojinao yake hayo kwa jeuri,amesema,anaelewa Sera hiyo ya China ya kuifanya Taiwan kuwa ni sehemu yake,lakini kwake msimamo huo utaendelea kwa sharti iwapo wataweka makubaliano katika mambo kadhaa ikiwemo Biashara.