CHAMA CHA WANASHERIA AFRIKA (PALU )NA TAASISI NYINGINE WAKUTANA ARUSHA KUJADILI MATUMIZI YA DIGITALI DUNIANI

6 years ago65 Views

Deonald Dea Afisa mtendaji mkuu wa chama cha Wanasheria wa Afrika (PALU)


Na.Vero Ignatus Arusha.

CHAMA CHA WANASHERIA AFRIKA (PALU )NA TAASISI NYINGINE WAKUTANA ARUSHA KUJADILI MATUMIZI YA DIGITALI DUNIANI

CHAMA cha Wanasheria wa Afrika (PALU) kwa kuahirikiana na Taasisi zingine ikiwemo inayosimamia matumizi ya kidijitali Duniani Article 19, wamekutana Jijini Arusha kwa ajili ya kujadili na kuweka mikakati ya kusimamia haki za watumiaji wa mitandao ya teknolojia ya kidijitali, ili kuwezesha wananchi wa nchi hizo kupata huduma.
Deonald Dea ni Afisa mtendaji mkuu wa chama PALU ambapo amesema kuwa, binadamu wana haki ya kupata huduma ya mawasiliano ya kidijitali ili waweze kuendesha shughuli za kibinadamu vizuri.
Deya alishauri badala ya serikali kukimbilia kufunga mitandao hiyo, wangeiachia Bunge lipitishe sheria nzuri za kusimamia suala hilo na huku Mahakama zikihakikisha zinapewa nafasi za kuhakikisha sheria hizo zinasimamiwa na anayekiuka anapata stahiki yake

Dea amesema kuwa Mawasiliano ni muhimu kwa wakati kama huu sababu mitandao inatumika katika kufanya biashara ,kutoa elimu na hata maswala ya Afya pamoja na mengine mengi.
“Sisi kama binadamu tuna uhuru wa kuzungumza na uhuru wa kupata taarifa sahihi na kwa mfumo wa sasa wa kutumia mawasiliano ya kidijitali kama Intenet ndio njia kubwa za kusambaza habari na hapo kuna sheria zinazotakiwa kuwepo ili kulinda uhuru huu kwa binadamu,”alisema”
Amesema wamekutana wanasheria, wanaharakati, toka nchi za EAC na Maofisa wa haki za binadamu wa jumuiya ya Afrika ya mashariki na Tume ya umoja wa Afrika ya kupambana na Rushwa ,na Mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu na kijamii .
“Kwani kweli hata serikali inatumia mitandao hii kufanikisha kukamata wahalifu wa makosa mbalimbali , hivyo vema kila upande ukaheshimu haki ya wengine na sio kukimbilia kuzuia wngine wasipate haki ya mawasiliano,”alisema 
Amesema kuwa pamoja na haki hizo bado zipo baadhi ya serikali ya nchi hizo zinakiuka haki za binadamu za uhuru wa kuhakikisha wanapata mawasiliano kwa kufunga mitandaobya kijamii wakihofia kukashifiwa jambo balo siyo sahihi
Ephraim Kenyanito kutoka Afisa mipango wa kidigitali kutka Article 19 ya nchini Kenya kuwa ni vyema kukawepo na sheria zitakazowasaidia wananchi kutumia vizuri teknoloji kuweza kupata mawasiliano ya haraka na kufanya biashara.
“Hadi sasa hatuwezi kuzifikia nchi zilizoendelea katika matumizi ya kidijitali kwenye masuala mbalimbali , hivyo vema na nchi zetu za EAC tukafanya jitihada kuweka mipango madhubuti ya kusimamia hili na kueneza huduma hizo za mtandao kwa wananchi wote wa nchi za EAC, na hasa vijijini,”alisema Mwisho
Amesema hivi sasa katika nchi nyingi wanawake wananwake hawajaunganishwa kutumia teknolojiankama wanaume hivyo watafiti watumie sheria jinsi ya kufanya ili watu watumie mitandao.

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2WtDTr7
via

Previous Post

Next Post

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.