Breaking Newzzz:Rais John Magufuli kuzuru Rwanda…itakuwa ndiyo ziara yake ya kwanza nje

Masama Blog9 years ago6 Views

MagufuliRais wa Tanzania John Magufuli amepangiwa kufanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi hiyo tangu kuingia madarakani mwaka jana.
Dkt Magufuli anatarajiwa kuzuru nchi jirani ya Rwanda Jumatano na Alhamisi, kufuatia mwaliko kutoka kwa Rais Paul Kagame.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wizara ya mambo ya nje ya Tanzania, Dkt Magufuli na Bw Kagame watafungua daraja la kimataifa la Rusumo na kituo cha huduma za pamoja mpakani katika mpaka wa Tanzania na Rwanda.
Kagame kuiga Magufuli katika matumizi
Baadaye, wataelekea Kigali ambapo watafanya mazungumzo ya pamoja.
Dkt Magufuli pia ataweka shada la maua katika makumbusho ya mauaji ya kimbari ya Rwanda 1994 mjini humo.
“Ikizingatiwa kwamba hii ndiyo ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu achukue madaraka Oktoba 2015, ziara hii inaashiria umuhimu ambao Tanzania inaweka katika kuimarisha uhusiano wake na majirani zake.”
Rais Magufuli amekuwa mapumzikoni nyumbani kwake eneo la Chato, kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.