BOZI AELEZA SABABU ZA KUTODUMU KWENYE MAPENZI

Admin Updates10 years ago6 Views

Muuza sura kwenye sinema za Kibongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’.


MUUZA sura
kwenye sinema za Kibongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ ambaye alikiri kubanjuka
na mastaa wasiopungua 15, amesema sababu zinazomsababisha asidumu na
mwanaume mmoja kwenye mapenzi ni kutokana na mateso aliyoyapata kwenye
ndoa ya utotoni.

Akibonga mawili matatu na paparazi wetu,  Bozi alisema tatizo la
kutokuwa na msimamo kwenye mapenzi linatokana na kuumizwa na mwanaume
ambaye alimuamini na kuingia naye kwenye ndoa, ambapo aliambulia vipigo
na mafumanizi ya mara kwa mara.

“Ukweli mshipa wa kupenda umeshanikatika, nikiwa na mwanaume kwa kipindi
kifupi tu namchukia na kusitisha uhusiano, chanzo kinatokana na
mwanaume ambaye alinibembeleza anioe nikiwa na umri wa miaka 17 tu na
kila siku kufuma SMS za wanawake na hata kumshuhudia, nilichoambulia ni
mtoto ambaye jukumu zima la malezi ni mimi mwenyewe,” alisema Bozi.

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.