BONGO MOVIES HILI LA UKIMWI MLITAZAME KWA JICHO LA TATU

Admin Updates10 years ago95 Views

Kwenu mastaa wa Bongo Movies, bila shaka mko poa na mnaendelea na
majukumu yenu ya kila siku. Nawapongeza kwa hilo maana kazi nzuri
tunaziona kila kukicha.Mkitaka kujua hali yangu mimi ni mzima wa afya,
kama kawaida naendeleza harakati zangu ndani ya mjengo wa Global
Publishers.

Leo nimewakumbuka kupitia barua sababu wengi wenu huwa hatupati muda wa
kuzungumza. Naamini kwa barua hii ujumbe utawafikia wengi kwa wakati
mmoja.Dhumuni la barua hii ni kutaka kuwakumbusha kuhusu suala zima la
ugonjwa wa Ukimwi (Ngoma). Hakuna asiyejua kwamba ugonjwa huu ni hatari
na unaua.

Ndugu zangu, nimeguswa kuwaandikia barua hii sababu ukweli ni kwamba
aina ya maisha yenu wengi wenu nayajua. Mara kwa mara tumekuwa tukisoma
kuhusu nyinyi kushea mabwana na mabibi kwenye magazeti yetu.
Hiyo inaonesha ni jinsi gani mpo katika hatari ya kupata maambukizi ya
ugonjwa huo. Kinachonisikitisha zaidi ni kwamba, mastaa wengi wa kike
wanaishi kwa kutegemea mabwana, hii ni hatari.

Kwa nini msifanye kazi zenu za kuigiza ambazo zimewapa umaarufu. Sanaa
si ndiyo imewafanya muwe maarufu? Kwa nini mnaamua kuiweka kando?Hamtaki
kufanya kazi, mnataka kugombea mabwana wenye nazo. Mbaya zaidi mabwana
wenyewe mnaowagombea ndiyo walewale, fulani anamuona mwenzake anatembea
na mtu fulani basi na yeye anamzunguka kwa tamaa ya fedha.

, Nasibu Abdul ‘Diamond’Hata huyo anayemzunguka mwenzake naye inafika
wakati anapokonywa na mtu mwingine. Katika mzunguko huo mmoja akiwa
muathirika basi wote mmekwenda na maji.

Baadaye msururu wa mabwana unahamia kwenda kwa mastaa wenzenu wa filamu,
nao kila kukicha mnabadilishana. Leo utasikia fulani anatembea na
fulani kesho amehamia kwa mwingine.Mastaa wa kiume wanatumia kigezo cha
kudai watawachezesha sinema wasanii wachanga, ngono zembe inatawala,
hakuna tena kuwapa hata hizo nafasi za kuigiza.

Jamani katika ulimwengu huu wa sasa si wa zama zile. Watu wanapaswa
kubadilika, kuishi kisasa, kujitambua afya na kujikinga.Elimu imetolewa
ya kutosha, hakuna mtu asiyejua. Kwa nini muendelee kufanya ngono zembe
wakati mnatambua madhara yake? Kwa nini tunayahatarisha maisha yetu
kiasi hiki? Tubadilike!

Mastaa wa kike badilikeni, fanyeni kazi msitegemee mabwana. Watanzania
waliwajua kupitia sinema na michezo ambayo mlikuwa mkiigiza, komaeni
kupitia kazi hizo za sanaa muweze kutengeneza kazi nzuri ambazo mtaziuza
ndani na nje ya nchi.

Tumechoka kusikia habari za kukwapuliana mabwana. Tuseme inatosha kufanya ngono zembe.
Ni matumaini yangu mmenielewa, nawatakia kazi njema!

Barua Nzito By Erick Evarist, Global

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.