Kwa mujibu wa benki hiyo huduma hiyo iliyozinduliwa jana ni mwendelezo wa juhudi za kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanatumia huduma za benki sambamba na kuhamasisha utunzaji fedha kwa njia salama na za uhakika.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama amesema kuwa huduma hiyo inaweka msingi wa kurasimisha sekta ndogo ya usafiri wa bodaboda.
“Mnachokifanya leo kina baraka zote za Serikali. Hiki kitawasaidia vijana kuongeza umakini kwenye shughuli zao na kuchangia uchumi wa Taifa,” amesema Mhagama.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna amesema huduma hiyo inatoa fursa kwa maelfu ya madereva wa bodaboda nchini kutumia huduma za benki hatua ambayo itaimarisha usalama wa fedha zao pamoja na wao wenyewe.
“Hii ni namna bora zaidi ya kurudisha uwajibikaji kwa shughuli za madereva wa bodaboda ambao mchango wao kwenye uchumi wa Taifa unatambulika,”amesema na kuongeza huduma hiyo itaanza kwa Jiji la Dar es Salaam kisha itaenda Mwanza, Arusha, Ruvuma, Dodoma na Mbeya wiki chache zijazo.
Zaipuna ameongeza kuwa mfumo huo wa malipo utawasaidia madereva bodaboda kukuza biashara zao kwa kuwapunguzia adha ya kuhifadhi fedha taslimu na kuwapa fursa ya kuepuka matumizi yasiyokuwa na mpangilio.
“Kwa kutumia MasterCard QR, tunatoa huduma ya uhakika wa malipo kwa madereva bodaboda kutoka kwa watoa huduma wote na benki za biashara wanaotumia huduma hii.
” Malipo yatafanywa kwa kutumia simu ya mkononi yenye programu ya MasterCard QR na kupunguza hatari za kumiliki fedha taslimu. Huduma hii kwa bodaboda ni sehemu ya mkakati wa benki kufikisha huduma zake kwa watu wengi zaidi,” amesema Zaipuna .
Wakati huo huo Mwakilishi wa MasterCard Tanzania Frank Molla amesema mfumo huo wa malipo ya kidijiti unakusudia kuwapa uhuru dereva na abiria wake wakati wote wa safari huku ukimuepushia dereva uwezekano wa kuporwa au kupoteza fedha zake.
“MasterCard inakusudia kuhamasisha na kuwezesha malipo ya kidijiti hapa nchini. Benki ya NMB inayo dira inayofanana nasi katika ujenzi wa miundombinu itakayoiwezesha jamii kufurahia ulimwengu wa malipo ya kimtandao kwa kutumia teknolojia ya kisasa,” amesema.
Tayari Benki ya NMB imewajengea uwezo zaidi ya madereva 1,000 wa jinsi ya kutumia QR kufanikisha malipo kwa kutumia simu za mkononi. Mfumo huo unatarajiwa kuongeza usalama wa malipo ya kimtandao kwa sekta hiyo ndogo ya watoa huduma.
Kumlipa bodaboda, abiria anatakiwa kwenda kwenye simu yako – NMB Mkononi, piga *150*66# kupata menu na kuchagua kufanya malipo halafu ‘Scan to Pay.’ Pia ukiwa na simu janja nenda kwenye programu (App) ya NMB Mkonini ambako atachagua ‘Scan to Pay’ na kuendelea na maelekezo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama akizungumza mbele ya wageni waalikwa na Waendesha piki piki kutoka sehemu mbalimbali ndani ya jiji la Dar,kabla ya kuzindua huduma ya Mastaboda,jana jijini Dar.Huduma hiyo ni maalum kwa waendesha boda boda.
Mgeni rasmi (wanne kushoto) ,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama akiongoza uzinduzi wa huduma hiyo ya Mastaboda,jana jijini Dar.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna akimshukuru Mgeni rasmi ,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama mara baada ya tukio la uzinduzi wa huduma hiyo kufanyika.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna akifafanua jambo mbele ya Waendesha piki piki (hawapo pichani),kuhusu huduma ya Mastaboda,alisema kuwa huduma hiyo inatoa fursa kwa maelfu ya madereva wa bodaboda nchini kutumia huduma za benki, hatua ambayo itaimarisha usalama wa fedha zao pamoja na wao wenyewe.
Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa hudma hiyo ya Mastaoda.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2OTz321
via






