Basi la kampuni ya Fikoshi linalofanya Safari zake kati ya Karagwe na Mwanza limegonga tembo usiku wa kuamkia leo katika eneo la Byenturege Kitengure Wilayani Karagwe lilipokuwa likitokea Mwanza.
Eneo hilo ni linatambulika kuwa ni Sehemu ambapo Wanyama tofauti kama Swala, Simba, Tembo ambao hupenda kukatiza Barabara wakati wakijitafutia chakula, licha ya kuwepo kwa alama na Vibao vya Tahadhali, lakini Magari yamekuwa yakipita kwa kasi katika eneo hilo na inaelezwa ndio sababu ya basi hilo kugonga Tembo. Hakuna binadamu aliyepoteza maisha katika ajali hiyo zaidi ya Tembo na Basi kuumia. Tutaendelea kukuletea taarifa zaidi hapo baadae.
Basi la Fikoshi linalofanya Safari zake kati ya Karagwe na Mwanza limegonga tembo usiku wa Jana eneo la Byenturege Kitengure Wilayani Karagwe likitokea Mwanza. Hakuna madhara mengine zaidi ya Basi kuumia. Tunaendelea kufuatilia.
from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2VNzrEa
via



