VITUKO kibao vilitawala juzikati kwenye sherehe ya
ujio wa mtoto wa staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel (Baby Shower),
baada ya mastaa na waalikwa kibao kuonekana kufanya vituko vya hapa na
pale.Licha
ya tukio hilo, pia waalikwa walicheza vyema muziki kwa shangwe na
furaha huku wakizungusha nyonga kwa ustadi wa aina yake.Waalikwa
waliokuwa wamevalia sare za aina mbili, walikuwa burudani ya aina yake
huku karibu wote, wakienda kulibusu tumbo la Aunt ambalo sasa limekuwa
kubwa kiasi cha kuonekana kuwa ni mtu wa kujifungua leo au kesho.
Tukio
hilo lilijiri usiku wa kuamkia Mei 10, mwaka huu katika Viwanja vya
Ndoto Polepole, huko Bagamoyo mkoani Pwani, ambako waalikwa walipata
fursa ya kula, kucheza na baadaye kutoa zawadi kwa ajili ya mtoto
atakayezaliwa.
Aunt Ezekiel alimtambulisha mpenzi wake, Moze Iyobo kwa kumlisha keki kabla ya kumwagiana mabusu na kunyonyana ndimi hadharani.
Akizungumza
kwenye hafla hiyo, Aunt alisema anashukuru marafiki na ndugu zake kwa
kuwezesha shughuli hiyo kufanyika, kwani awali aliamua aifanye baada ya
mtoto wake kuzaliwa.“Nimefurahi sana maana watu wamejitolea kwa hali na
mali na kubwa zaidi ni hii sehemu ambayo tumefanyia sherehe, kiukweli ni
mbali sana hivyo inanifanya kuamini kila aliyeweza kuja huku ana
mapenzi ya dhati na mimi,” alisema Aunt.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33





