

********************************
Na farida saidy morogoro
Jeshi La Polisi Mkoa wa Morogoro Benson Benard (31) aliekutwa Uchi wa Mnyama yeye na Mtoto wake katikati ya Maporomoko ya Maji eneo la Mlimani Nguzo Camp ndani ya manispaa hiyo na alipoamuliwa kuondoka eneo hilo hatarishi akajirusha na kujizamisha kwenye Maji yaliyokuwa wakitiririka kwa kasi kabla ya kushikiliwa na Polisi.
Aidha katika Eneo hilo la Tukio Askari Polisi walikuta Panga na Msumeno ambapo pia kunadaiwa kumefanyika uharibifu wa mabomba ya maji, na sasa mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano.
Hata hivyo Mtoto amekabidhiwa kwa mama yake mzazi Mary Shao mkazi wa Kihonda, ambae nae anasema muwewe alianza kubadilika kwa kuongea mambo yasiyo eleweka na siku hiyo ya tukio aliaga anaenda kuogelea.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2MhM1oh
via






