AFYA:Haya Hapa Madhara ya Kuzungumza na Simu Muda Mrefu

Admin Updates1 year ago4 Views

Januari 5, 2024, Dodoma

Na. Raymond Mtani BMH

Imeelezwa kuwa
kuzungumza kwa njia ya simu kwa muda mrefu kinaweza kuwa
chanzo
mojawapo cha kupoteza usikivu.
Hayo yamesemwa na Leonard Tibihika, Mtaalamu wa
Upimaji Usikivu wa Hospitali
ya Benjamin Mkapa (BMH) katika mahojiano
maalumu kuhusu huduma za

uchunguzi wa
Usikivu Hospitalini hapo, leo Januari 5, 2024.“isitafsirike vibaya, si kila
anayeongea na simu anahatarisha usikivu, bali yule
anayetumia muda mrefu
kuongea na simu, kwa sababu mgandamizo wa sauti
inayoingia sikioni
ukiendelea kwa muda mrefu huathiri Ngoma ya Sikio” Alisema

Tibihika.

Watu wengine
waliyoko katika hatari ya kupoteza usikivu ni wale wanaofanya kazi
katika
mazingira ya kelele, alisema Mtalaamu huyo akitolea mfano, wafanyakazi wa
viwandani
na wanaokesha kwenye klabu za muziki, na wale wenye shughuli katika
masoko.“changamoto
anayoweza kukutana nayo mtu anayepoteza usikivu ni kutogundua
mapema kuwa
usikivu wake hauko katika kiwango cha kawaida, akachukua hatua
kwa sababu
usikivu hupungua polepole wakati mwingine hadi ambiwe na wengine”

Tibihika.

Kuchelewa
kugundua kuwa usikivu unapotea, au kugundua na kutochukua hatua za
kuchunguzwa
ili kutibiwa husababisha watu wengi kufika Hospitali wakiwa katika
hatua mbaya
kiasi cha kuhatarisha kupoteza usikivu kabisa.
  Taarifa za Vituo vya Udhibiti na Kukinga Magonjwa (CDCs) zinadokeza
kuwa,


Watoto na Vijana
wadogo milioni 5.2 na watu wazima milioni 26 hupoteza uwezo wa
kusikia
kutokana na kuwa kwenye mazingira ya kelele.
Katika moja ya tafiti
kuhusu kupoteza usikivu kwa matumizi makubwa ya simu
uliyobandikwa katika
tovuti ya Shirika la Afya Duniani (WHO), unathibitisha kuwa

matumizi ya
zaidi ya dakika 60 kila siku yanaweza kuathiri usikivu wa binadamu

ndani ya miaka
5.

Tibihika, anatoa
wito kwa watumiaji wa simu kwa muda mrefu, kuchukua hatua za
kujikinga,
pamoja na kuhakikisha wanafanyiwa uchunguzi wa usikivu angalau mara
mbili ndani
ya miezi 12.
Hospitali ya Benjamin Mkapa, ni miongoni mwa Hospitali tatu za
serikali nchini
zinazotoa huduma za uchunguzi wa usikivu kwa kufanya vipimo vya aina
zote,
asilimia kubwa ya wagonjwa wanaopoteza usikivu hubainika kuwa na
tatizo la
kupasuka Ngoma ya Sikio.

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.